1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Papa Leo kutoa baraka maalum za Pasaka huko Vatican

5 Aprili 2026

Kiongozi wa kanisa Katoliki duniani Papa Leo XIV ( kumi na nne) ameongoza misa yake ya kwanza ya Pasaka kama Papa kwa kutoa wito wa tumaini dhidi ya ghasia za vita inayouwa na kuharibu.

https://p.dw.com/p/5BgqW
Vatican 2026 | uwanja wa mtakatifu Petro.
Papa Leo XIV aongoza ibada yake ya kwanza ya Pasaka kama kiongozi wa kanisa Katoliki duniani katika uwanja wa Mtakatifu Petro huko VaticanPicha: Matteo Minnella/REUTERS

Leo, papa wa kwanza mzaliwa wa Marekani, amehutubia waumini katika Uwanja wa Mtakatifu Petro huko Vatican uliopambwa kwa mawaridi meupe ambapo maelfu ya waumini walikusanyika .

Papa Leo aliwasihi waumini kudumisha matumaini mbele ya vifo, vinayonyemelea kupitia udhalimu, ubinafsi wa kibaguzi, katika ukandamizaji wa maskini na kutowajali wanyonge.

Baadaye atatoa ujumbe maalumu wa kitamaduni kwa wakazi wa Roma na duniani nzima unaojulikana kama Urbi et Orbi.

Kulingana na mafundisho ya Biblia, Pasaka husherehekewa kuadhimisha ufufuko wa Yesu Kristo.