1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Papa Leo aongoza Misa yake ya kwanza ya Jumapili ya Matawi

Saleh Mwanamilongo
29 Machi 2026

Papa Leo XIV ameanza wiki yake ya kwanza kabla ya Pasaka kwa kuongoza misa ya jadi ya Jumapili ya Matawi mbele ya maelfu ya waumini katika Uwanja wa Mtakatifu Petro mjini Roma.

https://p.dw.com/p/5BLOA
Vatican City 2026 | Misa ya Jumapili ya Matawi na Papa Leo XIV katika Uwanja wa Mtakatifu Petro
"(Yesu) hasikilizi sala za wale wanaoanzisha vita, bali huzikataa, Papa Leo akisema: "Hata mkitoa sala nyingi, sitasikia; mikono yenu imejaa damu,’ aliongeza akitoa dondoo la BibliaPicha: Pool/Catholic Press Photo/IPA/ZUMA/picture alliance

Kwenye hotuba yake Papa Leo alisema Mungu hasikilizi sala za viongozi wanaoanzisha vita na walio na "mikono iliyojaa damu".

Sherehe hii inaashiria mwanzo wa Wiki Takatifu, ambapo Wakristo hukumbuka mateso na kifo cha Yesu Kristo kabla ya kusherehekea ufufuo wake siku ya Pasaka. Hii ni Pasaka ya kwanza kwa Papa Leo XIV tangu achaguliwe Mei mwaka jana.

Katika ratiba yake, ataongoza ibada ya Alhamisi Kuu pamoja na ibada ya kuosha miguu, kisha kushiriki Ijumaa Kuu katika njia ya msalaba kwenye Ukumbi wa Colosseum.

Maadhimisho yatahitimishwa na misa kubwa ya Pasaka Jumapili, ikifuatiwa na baraka ya "Urbi et Orbi” kwa dunia nzima.