1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Papa leo awasili Angola kama sehemu ya ziara yake Afrika

18 Aprili 2026

Kiongozi wa kanisa katoliki duniani Pope Leo XIV amewasili Angola leo alasiri kwa ziara ya siku tatu katika nchi hiyo iliyo tajiri kwa mafuta lakini karibu theluthi mbili ya wananchi wake ni masikini.

https://p.dw.com/p/5CQPi
Angola Luanda 2026 | Papst Leo XIV na  João Lourenço
Kiongozi wa kanisa katoliki duniani Papa Leo XIV akilakiwa katika uwanja wa ndege wa Luanda na Rais wa Angola João Lourenço Picha: Guglielmo Mangiapane/REUTERS

Ndege ya kiongozi wa kanisa hilo ambaye ni wa kwanza kutokea Marekani, ilitua kwenye mji mkuu Luanda saa tisa alasiri.

Angola inakadiriwa kuwa na waumi milioni 15 wa kikatoliki ikiwa ni takriban asilimia 44 ya idiadi jumla ya watu nchini humo.

Papa Leo aliyeanzia ziara yake ya bara la Afrika nchini Algeria na Cameroon, anatarajiwa kukutana baadae na rais wa Angola Joao Lourenco kisha kutoa hotuba kwa umma.

Akizungumza na waandishi habari kabla ya kuanza safari yake ya Angola, Pape Leo XIV alisema anajutia matamshi yake ya kupinga vita duniani, kuchukuliwa kama ugomvi wa maneno na Rais wa Marekani Donald Trump, akisema hana muda wa kugombana na rais huyo.