Papa Leo akutana na viongozi wa Kikristo Mashariki ya Kati
28 Novemba 2025
Matangazo
Katika sherehe za maadhimisho ya miaka 1,700 ya baraza kuu la Kanisa lenye makasisi wakuu kutoka nchi zikiwemo Uturuki, Misri, Syria na Israel, zilizoandaliwa mjini Iznik ambao awali ulijulikana kama Nicaea, Papa Leo alisema ni kashfa kwamba Wakristo bilioni 2.6 duniani hawana umoja thabiti.
Kiongozi huyo wa kanisa Katoliki pia amesema kwasasa, ubinadamu wote ulioathirika kwa vurugu na mizozo unataka maridhiano na upatanisho.
Pia amesema lazima watu wapinge matumizi ya dini kuhalalisha vita, vurugu ama mfumo wowote wa kiitikadi na kuongeza kusema njia za kufuata ni mazungumzo na ushirikiano.