1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroPakistan

Pakistan yalaani matamshi ya "uchokozi" ya India

6 Aprili 2024

Pakistan, hii leo imelaani matamshi iliyoyaita ya uchokozi yaliyotolewa na Waziri wa Usalama wa India, Rajnath Singh.

https://p.dw.com/p/4eV8y
Waziri wa Ulinzi wa India, Rajnath Singh
Waziri wa Ulinzi wa India Rajnath Singh aliposhiriki mkutano wa pamoja wa wanahabari wakati wa Mazungumzo ya nne ya Mawaziri wa Marekani na India mjini Washington, DC, Aprili 11, 2022.Picha: MICHAEL MCCOY/AFP

Sing alinukuliwa akisema India itaingia Pakistan na kumuua yoyote atakayetoroka kupitia mpaka wake baada ya kujaribu kufanya mashambulizi ya kigaidi.

Singh alitoa matamshi hayo siku ya Ijumaa baada ya gazeti la Guardian kuchapisha ripoti iliyosema serikali ya India imewaua watu 20 nchini Pakistan tangu mwaka 2020, kama sehemu ya mpango wake mpana wa kuwalenga magaidi wanaoishi mataifa ya kigeni.

Pakistan ilisema mapema mwaka huu kwamba ilikuwa na ushahidi wa kuaminika unaowahusisha mawakala wa India na mauaji ya raia wake wawili nchini humo. India hata hivyo ilisema hizo ni "propaganda na uongo mtupu."