1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaHungary

Orban aushutumu upinzani kutaka kunyakua madaraka kwa nguvu

10 Aprili 2026

Waziri Mkuu wa Hungary Viktor Orban ameushutumu siku ya Ijumaa upinzani nchini humo akisema unajaribu kuvuruga uchaguzi wa Bunge utakaofanyika siku ya Jumapili.

https://p.dw.com/p/5C01F
Budapest 2026 | Waziri Mkuu wa Hungary Viktor Orban
Waziri Mkuu wa Hungary Viktor Orban akizungumza mjini Budapest alipompokea Makamu wa rais wa Marekani JD VancePicha: Jonathan Ernst/REUTERS

Orban aliye madarakani kwa miaka 16, amedai kuwa wapinzani wanashirikiana na idara za ujasusi za kigeni kuwatishia wafuasi wake kwa vurugu huku wakilenga kunyakua madaraka kwa nguvu.

" Wanaanza kulalamika kuhusu udanganyifu kwa shutuma za uongo hata kabla ya uchaguzi. Wanaandaa maandamano na machafuko hata kabla ya kura zenu kuhesabiwa. Hebu tuzungumze wazi! Hili ni jaribio lililopangwa la kutilia shaka uamuzi wa watu wa Hungary kupitia machafuko, shinikizo, na shutuma za kimataifa," alisema Orban.

Kulingana na kura za maoni,  Chama cha Fidesz  chake Orban ambaye ni mshirika wa Urusi na Marekani, kinatazamiwa kushindwa na kile cha mpinzani wake Peter Magyar kinachounga mkono Umoja wa Ulaya.