1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaIsrael

Nyumba ya mshambuliaji wa bunduki yabomolewa Israel

23 Mei 2023

Jeshi la Israel limebomoa hii leo nyumba ya mtu aliyefanya shambulio baya la bunduki katika mji wa pwani wa Tel Aviv karibu miezi mitatu iliyopita.

https://p.dw.com/p/4RiES
Palästina, Gaza, Raketenangriff Israel
Picha: IBRAHEEM ABU MUSTAFA/REUTERS

Nyumba hiyo iliyokuwa ya familia ya mshambuliaji imebomolewa kwa vilipuzi karibu na mji wa Ramallah eneo la Ukingo wa Magharibi, na ilikuwa kwenye ghorofa ya pili katika jengo lenye ghorofa nne. Uamuzi wa kuivunja umelazimisha wakaazi wengine pia kupoteza makazi yao.

Soma pia: Wapiganaji watatu Wakipalestina wauwawa na jeshi la Israel

Israeli hutumia ubomoaji wa nyumba kama adhabu na hatua ya kuzuia mashambulizi. Mashirika ya haki za binadamu yanachukulia aina hii ya adhabu ya jumla kama ukiukaji wa sheria ya kimataifa ya ubinadamu.

Kumekuwa kukishuhudiwa makabiliano kati ya jeshi la Israel na wapiganaji wa Kipalestina katika Ukingo wa Magharibi. Tangu mwanzoni mwa mwaka huu, Wapalestina 116 wameuawa kufuatia operesheni za jeshi la Israel.