1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaMamlaka ya Palestina

Netanyahu: Israel itaendelea na mpango wa kuishambulia Rafah

23 Machi 2024

Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu amesema wanajeshi wake wataendelea na mashambulizi ya ardhini kwenye mji wa Rafah bila kujali uungwaji mkono wa mshirika wake mkuu, Marekani.

https://p.dw.com/p/4e36M
Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu
Waziri Mkuu wa Israel Benjamin NetanyahuPicha: Maya Alleruzzo/AP/dpa/picture alliance

Netanyahu amemueleza waziri wa mambo ya nje wa Marekani Antony Blinken kwamba hakuna njia nyengine ya kuwashinda wanamgambo wa Hamas bila ya Israel kuingia mjini Rafah.

Blinken akiwa mjini Tel Aviv kwa mazungumzo, ameeleza kuwa oparesheni inayopangwa kufanya na jeshi la Israel mjini Rafah sio suluhu.

Soma pia: Israel yadai kuwashikilia wanamgambo 500 wa Kipalestina 

Zaidi ya nusu ya Wapalestina milioni 2.3 wametafuta hifadhi katika mji huo wa kusini ambako Israel inasema viongozi wa Hamas wamejificha.

Maafisa wakuu wa Israel na Marekani wanatarajiwa kukutana mjini Washington wiki ijayo, ambapo Marekani itapendekeza njia mbadala kwa Israel za kuwawinda wapiganaji wa Hamas bila ya shambulio kamili mjini Rafah.