1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
JamiiIsrael

Netanyahu abebeshwa lawama juu ya tukio la mkanyagano 2021

Tatu Karema
6 Machi 2024

Uchunguzi wa tume maalum umebaini kuwa waziri mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu ni wakulaumiwa kuhusiana na tukio la mkanyagano la mwaka 2021 ambapo mahujaji 45 wa Kiyahudi waliuawa.

https://p.dw.com/p/4dEf3
 Israel Tel Aviv | Waziri mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu
Waziri mkuu wa Israel Benjamin NetanyahuPicha: Ronen Zvulun/AFP/Getty Images

Ripoti ya tume ya uchunguzi kuhusu mkasa huo imesema kuwa waziri huyo mkuu ana wajibu wa kubainisha kwa vitendo yeye mwenyewe au kupitia utaratibu unaofanywa kwa niaba yake, masuala ambayo yanahitaji uangalizi wa ofisi yake na, ikibidi, muingilio wake, hasa katika masuala yanayohusiana na hatari kwa maisha ya binadamu.

Uchunguzi huo umegundua kwamba kuanzia mwaka 2008 hadi siku ya mkasa huo, ofisi ya Netanyahu ilikuwa imearifiwa mara kadhaa juu ya hatari zinazoweza kusababishwa na msongamano mkubwa wa watu wanaozunguka kaburi la kiongozi wa kidini wa kiyahudi Shimon Bar Yochai.

Soma pia: Netanyahu akaidi shinikizo la kimataifa 

Hata hivyo waziri huyo mkuu hakuchukua hatua mwafaka kushughulikia hali hiyo.

Katika ujumbe kupitia mtandao wa kijamii wa X, kiongozi wa upinzani Yair Lapid, amemtaka Netanyahu kujiuzulu na kuonya kuwa ni muda tu kabla ya kutokea kwa janga lingine.