1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaTaiwan

Ndege 36 za kijeshi za China zaonekana kisiwa cha Taiwan

22 Machi 2024

Wizara ya ulinzi ya Taiwan imesema leo kuwa ndege 36 za kijeshi za China zimeonekana karibu na kisicho hicho chenye utawala wa ndani katika muda wa saa 24 zilizopita - idadi hiyo ya ndege ikiwa kubwa zaidi mwaka huu.

https://p.dw.com/p/4e04Y
Ndege za kijeshi za China
Ndege za kijeshi za ChinaPicha: Hu Shanmin/Xinhua/picture alliance

Wizara ya ulinzi ya Taiwan imeongeza kuwa imegundua pia meli sita za jeshi la wanamajai karibu na kisiwa hicho na kwamba ndege za kijeshi 13 zimevuka ujia wa bahari ya Taiwan, unaotenganisha China na kisiwa hicho kinachotawaliwa kidemokrasia.

Soma pia: China yalaani ziara ya ujumbe wa Marekani, Taiwan 

China inadai kuwa Taiwan ni sehemu ya himaya yake.

Tangu kuchaguliwa kwa Rais Tsai Ing-wen mwaka 2016, Beijing chini ya utawala wa Rais Xi Jinping imezidisha azma yake ya kuungana tena na kisiwa hicho.