1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Taiwan yaripoti maputo manane katika anga zake

Amina Mjahid
10 Februari 2024

Wizara ya ulinzi ya Taiwan imesema imegundua maputo manane katika mlango wake wa bahari ndani ya saa 24 zilizopita

https://p.dw.com/p/4cFii
Taiwan
Taiwan yasema imegundua maputo manane katika mlango wake wa bahariPicha: ROC/ZUMA Wire/IMAGO

Mawili kati ya hayo yalishuhudiwa juu ya kisiwa hicho, saa chache kabla ya sherehe za sikukuu ya mwaka mpya nchini China.

Wizara ya ulinzi ya Taiwan imesema puto la kwanza lilionekana asubuhi ya jana Ijumaa na jengine jioni.

China, Marekani kuzungumzia suala la Taiwan

Taiwan ambayo China inadai ni eneo lake, licha ya Taiwan kulipinga hilo imekuwa ikilalamika kuanzia mwezi Desemba kuhusu maputo hayo, ikisema ni hatari kwa usalama wa anga na jaribio la vita vya kisaikolojia.