NATO yashambulia Tripoli
28 Mei 2011Matangazo
Mripuko mkubwa uliitikisa wilaya ya Bab Al-Aziziya, eneo lisilo mbali na katikati ya mji huo. Mripuko mwingine ulitokea dakika chache baadaye.
Huu ni usiku wa nne mfululizo, kwa eneo la mji huo kulengwa katika mashambulio katika ya anga.
Hapo awali, shirika la habari la Libya -JANA- lilisema kuwa maeneo yanayokaliwa na raia katika mkoa wa Al-Qariet ulioko kusini mwa mji mkuu wa nchi hiyo, yamekuwa yakilengwa na mashambulio hayo ya anga.