NAIROBI:Mlipuko waua mmoja na kujeruhi 31 | Habari za Ulimwengu | DW | 11.06.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

NAIROBI:Mlipuko waua mmoja na kujeruhi 31

Mlipuko umetokea mjini Nairobi leo asubuhi na kusababisha kifo cha mtu mmoja na kujeruhi takriban wengine 31.Chanzo cha mlipuko bado hakijajulikana ila kwa mujibu wa Kamishna wa polisi Mohamed Hussein Ali mlipuko ulisababishwa na kitu kilichobebwa na mtu.

Polisi wanaeleza kuwa uchunguzi wa kwanza unabaini kuwa mtu mmoja alijaribu kuingia mkahawa mmoja nao walinzi walijaribu kumzuia kuingia kwani alikuwa na mavazi ya kutatanisha.Haijulikani iwapo mtu huyo alihusika na mlipuko huo.Mlipuko huo umetokea kwenye duka moja katika Hoteli ya Ambassadeur.Hoteli yenyewe haikuathirika.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com