Mwanamke ajiripuwa na kuuwa watu 16 Iraq | Habari za Ulimwengu | DW | 07.12.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

Mwanamke ajiripuwa na kuuwa watu 16 Iraq

BAQUBA

Mshambuliaji wa kike wa kujitolea muhanga ameuwa watu 16 leo hii wakati alipojiripuwa kwenye ofisi ya kundi linalopiga vita Al Qaeda katika jimbo la Diyala ikiwa ni siku chache baada ya kundi moja la vita takatifu vya Jihad kuonya juu ya mashambulizi mapya ya miripuko ya mabomu nchini Iraq .

Mripuko huo kwenye mji wa Muqdadiyah ulioko kilomita 100 kaskazini mwa Baghdad umejeruhi watu 27.

Polisi imesema mwanamke huyo ameripuwa mabomo yaliyopachikwa nguoni mwake katika ofisi ya kundi la Uamsho la Wasunni waliobeba silaha kupambana na kundi la Al Qaeda katika jimbo la kati la Diyala.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com