1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaUfaransa

Mtu mmoja afariki na 6 wajeruhiwa mjini Paris

Saleh Mwanamilongo
4 Mei 2024

Polisi imesema mtu mmoja ameuawa na sita kujeruhiwa usiku wa kumkia leo katika kitongoji cha kaskazini mwa mji mkuu wa Ufaransa, Paris, katika ufyatuaji risasi unaohusishwa na ulanguzi wa dawa za kulevya.

https://p.dw.com/p/4fVF3
Ripoti za ufyatuaji risasi unaohusishwa na ulanguzi wa dawa za kulevya mjini Paris
Ripoti za ufyatuaji risasi unaohusishwa na ulanguzi wa dawa za kulevya mjini ParisPicha: Luc Auffret/Anadolu/picture alliance

Waendesha mashitaka na meya wa mji huo wamesema mashambulizi hayo yalitokea mwendo wa saa sita usiku katika eneo la kuegesha magari karibu na kituo cha maonesho ya kitamaduni cha Sevran.

Baada ya kufika eneo la tukio, polisi waliwakuta majeruhi wanne wakiwa wamelala chini. Mmoja kati yao alifariki muda mfupi baadaye na wengine watatu kupelekwa hospitalini wakiwa katika hali mbaya.

Polisi imesema watu wawili walifika kwenye kituo hicho cha kuegesha magari na mmoja wao alishuka na kufyatua risasi na kisha washambuliaji kukimbia.