1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mpinzani mkuu Senegal akabiliwa na kesi ya ubakaji

Sudi Mnette
29 Aprili 2023

Kiongozi wa upinzani nchini Senegal Ousmane Sonko atafikishwa mahakamani Mei 16 kwa tuhuma za ubakaji, wakili wa mshtaki wake El Hadji Diouf ameyasema hayo leo hii, akithibitisha ripoti za vyombo vya habari vya nchi hiyo

https://p.dw.com/p/4QiNb
Ousmane Sonko
Picha: Fatma Esma Arslan/AA/picture alliance

Mwanasiasa huyo liyeshika nafasi ya tatu katika uchaguzi wa urais wa Senegal mwaka 2019,  amepanda kisiasa kwa kasi kutokana na umaarufu wake miongoni mwa vijana. Sonko, amteangaza atawania urais kwenye uchaguzi wa 2024.Hata hivyo, amejikuta kwenye mkono wa sheria mara kadhaa na alishtakiwa kwa tuhuma za ubakaji na mfanyakazi wa saluni aliyokuwa amekwenda kwa ajili ya kukandwa viungo.Sonko, mwenye  miaka 48, na mkaguzi wa zamani wa kodi, amekanusha shtaka hilo na kusema yeye ni mwathirika wa njama ya Rais Macky Sall akitaka kumuondoa katika kinyang'anyiro cha urais cha 2024.