Moscow. Ndege yatua kwa dharura. | Habari za Ulimwengu | DW | 28.12.2006
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

Moscow. Ndege yatua kwa dharura.

Ndege ya shirika la ndege la Russia Aeroflot imetua kwa dharura katika uwanja wa ndege wa kimataifa katika mjini wa Prague leo baada ya mtu mmoja kutishia kuilipua.

Ndege hiyo , ambayo ilikuwa inasafiri kutoka Moscow kwenda Geneva ikiwa na abiria 170, ililazimika kwenda katika eneo la pekee katika uwanja huo.

Wasafiri wanaripotiwa kuwa walifanikiwa kumkamata mtu huyo, ambaye alikabidhiwa kwa polisi wa Jamhuri ya Cheki.

Polisi wamelieleza tukio hilo kuwa ni jaribio la kuiteka nyara ndege lakini vyombo vya habari vya Russia vimewanukuu maafisa wakisema kuwa abiria huyo alikuwa amelewa.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com