1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

MONTREAL:Aliyebakwa akutana na mbakaji wake

23 Mei 2007
https://p.dw.com/p/CBzP

Mwanamke mmoja wa Rwanda kwa mara ya kwanza toka mauaji ya halaiki ya mwaka 1994 nchini humo, ameonana ana kwa ana na mtu anayemtuhumu kumbaka.

Mwanamke huyo alikutana na mtu huyo, Desire Munyaneza katika mahakama ya Quebec nchini Canada.

Munyaneza anashtakiwa chini ya sheria mpya ya uhalifu wa kivita na uhalifu dhidi ya haki za binadamu.

Mwanamke huyo alisema kuwa alibakwa mara tano na Munyaneza wakati alipojificha katika nyumba yao kukimbia wauaji wa kihutu.

Munyaneza ambaye alikataliwa ombi la hifadhi ya ukimbizi, alikamatwa mwaka juzi akituhumiwa kuendesha vitendo vya ubakaji, mauaji na utekaji nyara, wakati wa mauaji hayo ya halaiki.Kiasi cha Watutsi laki nane waliuawa.