Mkuu wa Adidas asema Platini anafaa kuwa rais wa FIFA | Michezo | DW | 10.07.2015
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Michezo

Mkuu wa Adidas asema Platini anafaa kuwa rais wa FIFA

Herbert anasema Platini ndiye mgombea bora kwa sababu analiongoza Shirikisho la Kandanda Ulaya – UEFA iliyo na vilabu imara na dimba maarufu na bora kabisa la Champions League

.Anaongeza kuwa Mfaransa huyo amefanya kazi nzuri katika mihula yake miwili aliyokuwa uongozini. Adidas ni mfadhili mkuu wa mchezo wa kandanda. Herbert anasema ikiwa Platini ataamua kugombea urais wa FIFA, mkuu wa SHirikisho la Kandanda la Ujerumani – DFB Wolfgang Niersbach anaweza kugombea nafasi ya kumrithi katika shirikisho la UEFA.

Platini aliamua kutogombea dhidi ya Blatter katika uchaguzi wa FIFA lakini huenda akawa mgombea sasa. Amekuwa mkuu wa UEFA tangu 2007 na alichaguliwa kuongoza kwa muhula wa tatu mapema mwaka huu. Niersbach ni mwanachama wa kamati kuu za UEFA na FIFA.

Mwandishi: Bruce Amani/AFP/reuters/DPA
Mhariri: Mohammed Abdul-Rahman