Mkutano wa siri baina ya Netanyahu na John Kelly | NRS-Import | DW | 20.02.2017
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

NRS-Import

Mkutano wa siri baina ya Netanyahu na John Kelly

Netanyahu alishirika katika mkutano wa siri na waziri wa zamani wa mambo ya nje John Kerry mjini Agaba Jordan mwezi wa Februari mwaka jana.

Washington Israle Min isterpräsident Netanjahu bei Pk mit Trump (picture-alliance/newscom/P. Benic)

Waziri mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu

Mkutano huo uliohudhuriwa  pia na mfalme Abdallah II wa Jordan na rais wa Misri Abdel Fattah el Sissi,  ulipendekeza kutafuta amani baina ya Israel na Palestina. Lakini Netanyahu, alilikataa pendekezo hilo ambalo liliungwa mkono na nchi za kiarabu. Kutokana  na maafisa wa utawala wa rais wa zamani Barack Obama, Kerry alipendekeza  nchi za mashariki  ya kati kuitambua Israel kama dola la kiyahudi. Lakini Netanyahu alikata pendekezo hilo, ambalo lingelazimisha Israel kuondoka katika sehemu ambazo tayari zinamilikiwa  na Israel .

Katika mageuzi yaliopendekezwa katika mkutano huo, nipamoja na yale ya nchi za kiarabu  kutambua kuwa Israel ni dola la kiyahudi, kutambua pia kuwa Jerusalem ni mji mkuu wa pande zote mbili yaani Israel na Palestina  na haki ya kurejea kwa wakimbizi wa  kipalestina katika maeneo waliyoyapoteza ndani ya kile kinachojulikana hii leo kama taifa la Israel. Mjumbe mmoja alisema kuwa sababu kubwa ya mkutano huo ilikuwa kuanzisha tena  mazungumzo ya amani ya mashariki ya kati ambayo Netanyahu mwenyewe alitaka yawepo .

Juhudi zilizopendekezwa katika mkutanohuo wa siri

Juhudi hizo pia zilionekana  kuwa msingi wa mazungumzo yaliodumu muda mfupi na Kiongozi wa upinzani mwenye msimamo wa wastani Isaac Herzog alipokuwa ajiunge na serikali ya Netanyahu. Lakini mpango huo ukavunjika haraka, wakati Netanyahu alipomjumuisha katika serikali yake kiongozi mwenye msimamo wa Kizalendo wa siasa kali za mrengo wa kulia Avigdor Lieberman na kumpa uwaziri wa ulinzi.

Netanyahu hakuzungumzia kabisa ripoti hiyo ya mkutano huo wa siri katika mkutano wake wa kila wiki na  baraza lake la mawaziri, na ofisi yake pia imekataaa kusema chochote juu ya mkutano huo .

Katika mkutano wake wa  kwanza na Rais wa Marekani Donald  Trump mjini Washington , Netanyahu  alisema kuwa

USA Israel | Benjamin Netanjahu bei Donald Trump in Washington (Reuters/K. Lamarque)

Benjamin Netanyahu na raisi wa marekani Donal Trump mjini Washington

" Kuna siku mpya na ni siku nzuri ."  Akimaaanisha mapokezi mazuri aliyoyapata alipofika Ikula ya White House. Lakini  mara hali hio ilibadilika pale tuTrump alipomuomba Netanyahu kusimamisha  kwa muda kidogo ujenzi wa makaazi ya kiyahudi katika sehemu zinazokaliwa  na Israel  katika maeneo ya wapalestina. Waziri wa ulinzi wa Israel Lieberman, alisema kuwa kwake yeye kuundwa dola ya Palestine ndio suluhisho muafaka.

"Mtazamo wangu ni kumaliza mgogoro huu na suluhuu ni kuwepo kwa dola mbili-Israel na Palestina . Naamini ni muhimu kwetu  kuwepo kwa dola yaa kiyahudi ," . Libermann aliyasema hayo wakati akihutubia mkutano wa  usalama mjini Munich mwishoni mwa juma lililopita.

 

Mwandishi :  Najma Said/APE /EAP

Mhariri       :  Mohammed Abdul-Rahman

 

   

Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com