1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaItaly

Mkutano kati ya Meloni na viongozi wa Afrika waanza Rome

Saumu Mwasimba
29 Januari 2024

Mkutano wa kilele kati ya waziri mkuu wa Italia na viongozi wa bara la Afrika umefunguliwa leo mjini Roma ukiwa na lengo la kuufafanua mpango mkubwa wa maendeleo wa Italia kuelekea bara hilo la Afrika.

https://p.dw.com/p/4bnw3
Waziri mkuu wa Italia Giorgia Meloni akiwa na Rais wa Msumbiji Filipe Nyusi
Waziri mkuu wa Italia Giorgia Meloni akiwa na Rais wa Msumbiji Filipe NyusiPicha: REMO CASILLI/REUTERS

Serikali ya Meloni inataraji mpango wake huo utapunguza wimbi la wahamiaji,kutanua vyanzo vya nishati pamoja na kuanzishwa mahusiano mapya kati ya Ulaya na Afrika. 

Viongozi wa juu kadhaa wa nchi za Afrika pamoja na Umoja wa Ulaya, Umoja wa Mataifa na wawakilishi wa taasisi za fedha za kimataifa wanashiriki mkutano huo wa Rome.

Hata hivyo mwenyekiti wa tume ya Umoja wa Afrika Moussa Faki Mahamat ameupokea kwa tahadhari mpango wa Italia kwa kuuambia mkutano huo wa kilele kwamba nchi za Afrika zingependelea zaidi kushauriwa kwanza kuhusu mpango huo kabla ya Italia kuuanzisha.

Faki ambaye aliwahi kuwa waziri mkuu wa Chad ameuambia mkutano huo kwamba Waafrika hawafurahishwi na ahadi ambazo haziendelezwi.