Mjerumani atekwa nyara kaskazini mwa Somalia | Habari za Ulimwengu | DW | 12.02.2008
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Habari za Ulimwengu

Mjerumani atekwa nyara kaskazini mwa Somalia

Raia mmoja wa Ujerumani anayefanyakazi na shirika la kutoa misaada kaskazini mwa Somalia, ametekwa nyara leo. Shirika la misaada la kijerumani la Deutsche Welthungerhilfe, limethibitisha utekaji nyara huo. Kwa mujibu wa wakaazi wa eneo la Erigabo, lililo takriban kilomita 900 kaskazini mwa mji mkuu Mogadishu, dereva wa mfanyakazi huyo amejeruhiwa wakati wa uvamizi uliofanywa na watu waliokuwa wamejihami na silaha. Wizara ya mashauri ya kigeni ya Ujerumani mjini Berlin inachunguza habari za kutekwa nyara kwa mjerumani huyo. Mwishoni mwa mwezi Disemba mwaka jana, wafanyakazi wawili wa kigeni wa shirika la misaada la madaktari wasio na mipaka, walitekwa nyara kaskazini mwa Somalia, lakini wakaachiwa baada ya juma moja.
Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com