Michelle Obama asema Trump hafai kuiongoza Marekani | Matukio ya Kisiasa | DW | 18.08.2020
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Marekani

Michelle Obama asema Trump hafai kuiongoza Marekani

Chama cha Democratic kimefanya kongamano lake la kwanza mwaka huu. Msemaji mkuu Michelle Obama mke wa aliyekuwa rais wa Marekani aliyataja mapungufu ya rais Trump kwa maneno makali.

Bi Michelle Obama mke wa rais wa zamani wa Marekani alizindua mkutano huo kwa kuelekeza mashambulio ya kumkosoa Rais Donald Trump na pia aliitumia fursa hiyo kumpigia upatu mgombea wa chama Democrats Joe Biden atakae kiwakilishachama hicho katika uchaguzi wa mwezi Novemba. Bi Obama amsema ili kumaliza misukosuko iliyosabbaishwa katika kipindi cha miaka minne ya utawala wa rais Trump ni lazima wamarekani wamchague Biden.

Katika hotuba ya bi Michelle Obama kwenye usiku wa kwanza wa mikutano ya kitaifa ya chama cha Democtrats bi Obama alisema rais Trump wa chama cha Republican alipata muda wa kutosha kuthibitisha kuwa anaweza kufanya kazi ya kuliongoza taifa lamarekani lakini hata hivyo ameshindwa kutatua mambo mengi na hasa katika wakati huu ambapo nchi inakabiliwa na janga la corona, matatizo ya kiuchumi pamoja na dhulma za ubaguzi wa rangi. Bi Obama amemtaja rais Trump kuwa ni rais mbaya kwa nchi ya Marekani.

Michell Obama pia alielezea kwamba rais aliyemaliza muda wake Barack Obama alifanikisha kupatikana huduma ya afya kwa watu wapatao milioni 20. Amesema utawalawa Obama uliheshimiwa ulimwenguni kotena kwamba utawalawa Obama uliweza kuwaakusanya washirika wa Marekani katika kukabiliana na mabadiliko ya hali ya hewa.

Kushoto: Joe Biden mgombea wa urais wa chama cha Democratc. Kulia: Kamala Harris mgombea mwenza wa chama cha Democratic nchini Marekani katika uchaguzi wa 2020.

Kushoto: Joe Biden mgombea wa urais wa chama cha Democratc. Kulia: Kamala Harris mgombea mwenza wa chama cha Democratic nchini Marekani katika uchaguzi wa 2020.

Bi Obama amesema viongozi wa Marekani wakati wa rais Obama na makamu wake Joe Biden walishirikiana na wanasayansi kusaidia kuzuia mlipuko wa Ebola usigeuke na kuwa janga la ulimwengu, lakini miaka minne baadaye, hali ya taifa hili ni tofauti sana. Zaidi ya watu 150,000 wamekufa, na uchumi wetu uko katika hali mbaya kwa sababu ya maambukizi ya virusi vya corona ambayo rais huyu aliyapuuza kwa muda mrefu sana.

Hotuba hiyo ya Michelle Obama ilikuwa ndefu kuwahi kutolewa kwenye historia ya mikutano ya chama cha Democratic na hiyo ni kutokana na umaarufu wa mwanamke huyo katika chama chake. Mgombea wa kujitegemea Bernie sanders pia alihudhuria mkutano huo wa chama cha Democrats.

Chanzo:/AP