Mdahalo wa chama cha Democratic wamuangazia zaidi rais Donald Trump | Matukio ya Kisiasa | DW | 01.08.2019
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Matukio ya Kisiasa

Mdahalo wa chama cha Democratic wamuangazia zaidi rais Donald Trump

Wanao wania urais kutoka Chama cha Democratic wamefikisha tamati mdahalo wao wa pili kwa kuelekeza mashambulizi yao dhidi ya Rais Donald Trump. Wagombea wote kumi wamemtaja rais Trump kuwa mpinzani wao mkuu.

Aliyekuwa naibu rais Joe Biden, amesema kuwa uchaguzi wa mwaka 2020 ni ''kinyang'anyiro cha roho ya Marekani''

Seneta Kamala Harris amemtaja rais huyo kuwa mviziaji na muoga na kusema yeye ndiye anayestahili kuchaguliwa kukabiliana naye katika uchaguzi ujao. Seneta Cory Booker anasema kuwa mzozo wa taifa hilo ni Donald Trump lakini sio tu Donald Trump. Booker ameongeza kuwa kumshinda Trump ni sakafu tu na wala sio paa.

Seneta wa California Kamala Harris amesema kuwa Donald Trump anashtahili kuchukuliwa hatua kwa kile anachokiona kuwa makosa 10 yanayostahili kufunguliwa mashtaka kutokana na ripoti ya mchunguzi mkuu Robert Mueller ya muingilio wa Urusi katika uchaguzi wa mwaka 2016. Harris amesema hayo Jumatano wakati wa majadiliano ya kumng'atua mamlakani rais wa nchi hiyo katika mjadala wa Detroit.

Wakati huo huo, aliyekuwa waziri wa nyumba Julian Castro amesema kuwa ushahidi uko wazi,'' Seneta wa New Jersey Cory Booker anatoa wito kwa wabunge kuanza harakati za kumng'atua mara moja:'' Meya wa mji wa New York Bill Blasio ametoa ilani ya tahadhari na kusema anaunga mkono hatua hiyo ya kumng'atua rais mamlakani lakini maafisa waliochaguliwa hawapaswi kuzingatia zaidi mjadala huo na kupuuza masuala yanayowahusu raia.

Seneta wa New York Kirsten Gillibrand anamshtumu Joe Biden kwa kupinga mkopo wa ushuru wa miongo kadhaa kwa akina baba na mama wanaofanya kazi. Gillibrand anapendekeza kuwa hiyo inamaanisha Biden alipinga wanawake kufanya kazi nje ya nyumba zao.

Biden amejibu kwa kusema ,''hiyo ilikuwa kitambo sana'': Kwa sasa anasemaanaunga mkono mkopo wa ushuru wa dola elfu 8 kwa familia zinazofanya kazi.

Gillibrand aliendelea kushinikiza na kumlazimu Biden kusema kuwa awali alisafiri naye kupigia debe kazi yake kuunga mkono malipo sawa kwa wanawake.

Wakati wa mjadala huo, Julian Castro alikuwa mwaniaji wa pili wa urais wa chama cha Conservative kumtaja rais Donald Trump kama mbaguzi wa rangi.

Julian Castro aliyekuwa waziri wakati wa uongozi wa Obama , alikuwa miongoni mwa wawaniaji kadhaa waliokuwa wakimshtumu Trump kuhusiana na suala hilo la ubaguzi.

Seneta Kirsten Gillibrand amesema anajihisi kujukumika kama mwanamke mzungu kupinga ubaguzi wa rangi katika taasisi. Ameongezea kuwa sio tu jukumu la wawaniaji wawili weusi amba.o ni Seneta Kamala Harris na Cory Booker kuzungumzia kuhusu ubaguzi.

Rais Donald Trump na baadhi ya wawaniaji wa urais wanaoongoza wa chama cha Democratic ndio waliolengwa katika taarifa za ufunguzi katika usiku wa pili wa mijadala ya Detroit.