Mayweather na Pacquiao kupanda ulingoni | Michezo | DW | 02.05.2015
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Michezo

Mayweather na Pacquiao kupanda ulingoni

Mji wa Las Vegas umejiandaa kwa pigano lililosubiriwa kwa muda mrefu kati ya Floyd Mayweather na Manny Pacquiao na uwavutia mashabiki wa michezo kote ulimwenguni

Mabondia hao wawili walikutana uso kwa uso katika zoezi la kupima uzani hapo jana mbele ya mashabiki waliofurika katika ukumbi wa MGM Grand Garden ambako pigano hilo litaandaliwa.

Pigano hilo la uzani wa Welterweight ambalo limekuwa jikoni likiandaliwa kwa zaidi ya miaka mitano limeuiweka mchezo wa ndondi katika kiwango cha juu kabisa, katika njia ambayo haijawahi kuonekana kwa miongo kadhaa.

Wakizungumza katika kikao cha waandishi wa habari, wanamsumbwi hao waliahidi kuwapa mashabiki wa ndondi tamasha la kukata na shoka. Kwanza ilikuwa zamu ya Pacquiao

Mashabiki wengi ulimwenguni watakesha ili kuwa sehemu ya pigano hilo la kihistoria, ikiwa ni pamoja na mji anaotokea Pacquiao kusini mwa Ufilipino.

Wafilipino wanamchukulia Paqcuiao kuwa shujaa wa taifa, na maelfu ya mashabiki watafurika katika kumbi za mazoezi na mabustani kutazama pigano hilo kwenye televisheni kubwa bila malipo kote mjini Manila na mikoa mingine. Na duka moja la keki nchini humo limetengeneza keki kwa mfano wa Manny Pacquiao ambayo inatoshana na bondia huyo, ili kusherehekea pigano lake

Pigano hilo kati ya Mayweather na Pacquiao katika ukumbi wa MGM Grand Garden mjini Las Vegas linatarajiwa kuwa kubwa zaidi kwa upande wa mapato katika historia ya mchezo huo.

Mwandishi: Bruce Amani/AFP/AP/DPA/Reuters
Mhariri: Mohamed Daman