1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroIran

Marekani yaanzisha upya mashambulizi nchini Iran

9 Julai 2026

Marekani imefanya mashambulizi mapya ya anga dhidi ya Iran mapema leo, hatua iliyojibiwa na Iran kwa kuyalenga mataifa ya Bahrain, Kuwait na Qatar.

https://p.dw.com/p/5GmsL
Mlango-Bahari wa Hormuz wa Iran 2026 | Boti ya kasi ya Walinzi wa Mapinduzi inakaribia meli ya mizigo
Iran inasema inayo mamlaka ya kudhibiti usafiri kwenye Mlango Bahari wa HormuzPicha: Meysam Mirzadeh/Tasnim News Agency/AP Photo/picture alliance

Marekani imefanya mashambulizi mapya ya anga dhidi ya Iran mapema leo, hatua iliyojibiwa na Iran kwa kuyalenga mataifa ya Bahrain, Kuwait na Qatar. Hali hii inaongeza mvutano na kuhatarisha tena makubaliano ya muda yaliyolenga kutafuta njia ya kumaliza vita.

Jeshi la Marekani lilishambulia maeneo mbalimbali ya kijeshi na miundombinu ya bandari mapema Jumatano, kufuatia mashambulizi ya Iran dhidi ya meli kadhaa za biashara katika pwani ya Oman, hali iliyosababisha Iran kujibu kwa mashambulizi mengine.

Mashambulizi ya Marekani yalifanywa saa chache baada ya Rais wa Marekani Donald Trump kusema makubaliano hayo yamefika mwisho kufuatia mashambulizi hayo ya Iran.

Hata hivyo, mashambulizi ya Alhamisi yalionekana kuwa makubwa zaidi kuliko ya awali huku Jeshi la Kuwait likisema limezuia na kudungua droni pamoja na makombora yaliyoelekezwa nchini humo.

Vyombo vya habari vya serikali ya Iran viliripoti milipuko katika maeneo kadhaa, yakiwemo Bushehr, ambako kuna kituo cha nishati ya nyuklia cha Iran, pamoja na miji ya bandari ya kusini ya Chabahar, Konarak, Bandar Abbas na Sirik.