1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroUkraine

Moscow yalaani maamuzi ya NATO ya kuisaidia kijeshi Ukraine

9 Julai 2026

Urusi imelaani maamuzi ya jumuiya ya NATO ikisema yanaweza kuwa na athari mbaya kabisa, baada ya muungano huo kutangaza msaada wa kijeshi kwa Ukraine na kuthibitisha tena dhamira ya wanachama kulindana.

https://p.dw.com/p/5Gmrn
NATO-Mkutano wa kilele 2026 | Picha ya pamoja ya wakuu wa nchi na serikali mjini Ankara
Urusi imekosoa vikali maazimio ya NATO ya kuendelea kuisaidia Ukraine Picha: Jonathan Ernst/REUTERS

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Urusi, Maria Zakharova, amesema inasikitisha, kuona NATO inachukua uamuzi kama huo bila kutafakari kwa kina ambao kulingana naye, yanaweza kusababisha janga si kwa muungano huo pekee, bali kwa dunia nzima.”

Katika mkutano wa kilele wa muungano huo nchini Uturuki jana Jumatano, nchi wanachama wa NATO ziliahidi kutoa yuro bilioni 70 kama msaada wa kijeshi kwa Ukraine kwa mwaka 2026.

Pia zilithibitisha tena "dhamira yao isiyotetereka” ya ulinzi wa pamoja chini ya Kifungu cha 5 cha Mkataba wa NATO, kupitia tamko la mkutano huo, na kutangaza mikataba ya silaha yenye thamani ya angalau dola bilioni 50.