1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Marekani imejikita katika kuondoa vikosi vyake Afghanistan

23 Agosti 2021

Makamu wa rais wa Marekani Kamala Harris amesema nchi yake inajielekeza zaidi katika hatua ya kuwaondoa raia wake na baadhi ya Waafghanistan walioko hatarini.

https://p.dw.com/p/3zN0H
Singapur | Kamala Harris und Lee Hsien Loong
Picha: Evelyn Hockstein/AP Photo/picture alliance

Kamala Harris ameongeza kwamba kutakuwa na muda wa kutosha wa kufanya tathmini ya zoezi zima linapohusika suala la kuondowa wanajeshi wake nchini humo.

Akizungumza na waandishi wa habari katika ziara yake nchini Songapore Kamala Harris amesema Marekani haipaswi kuvurugwa na hoja za nini kilikwenda mrama katika harakati za kuwaondoa raia na vikosi vyake nchini Afghanistan. Soma  Afghanistan: Watu saba wafariki katika mtafaruku nje ya uwanja wa ndege wa Kabul

Harris yuko nchini Singapore ambako amekutana na  waziri mkuu wa Lee Hsien Loong kwa mazungumzo juu ya masuala ya kuboresha uhusiano kati ya mataifa hayo mawili pamoja na juhudi za kudhibiti ukuaji wa kiuchumi na ushawishi wa kiusalama wa China.

Aidha viongozi hao watajadiliana kuhusu janga la Covid-19, usalama wa mtandaoni na ushirikiano.

Alipoulizwa na waandishi wa habari wa Singapore  kipi kilikwenda mrama wakati wa kuviondoa vikosi vya Marekani nchini Afghanistan Harris alijibu kwa kusema "Naelewa na kushukuru kwa nini unauliza swali hilo na nadhani kutakuwa na wakati mwingi wa kutathmini kile kilichotokea na kile kilichofanyika katika muktadha wa kuondoka Afghanistan. Lakini sasa hivi, tumejikita katika kuwaondoa raia wa Marekani, Waafghani ambao walifanya kazi na sisi na Waafghan ambao ni wanyonge, pamoja na wanawake na watoto." Soma Zoezi la kuwahamisha watu kutoka Afghanistan bado ni gumu

Rais wa Marekani Joe Biden amekosolewa kwa jinsi alivyolishughulikia swala la kuviondoa vikosi vyake kuanzia Marekani na hata kimataifa zoezi hilo likitajwa kuwa la vurugu baada ya kundi la Taliban kuchukua udhibiti nchini Afghanistan.

Singapur | Kamala Harris und Lee Hsien Loong
Kamala Harris na Lee Hsien LoongPicha: Evelyn Hockstein/REUTERS

Hata hivyo waziri mkuu Lee ameunga mkono uamuzi wa Marekani kujiondoa na kusema kuwa Singapore inashukuru kwa juhudi za Marekani za kupambana na ugaidi nchini Afghanistan.

Lee amesema wanatarajia kwamba Afghanistan haitakuwa kitovu cha ugaidi tena na kuongeza kuwa taifa lake litatuma ndege nchini Afghanistan kusaidia katika zoezi hilo la uokoaji.

Sehemu ya majukumu ya Harris katika ziara hii ni kuwaashawishi viongozi wa Singapore na Vietnam kuona kwamba   ushirikiano wa Marekani katika mataifa ya kusini mashariki mwa Asia ni dhabiti na hauwezi kulinganishwa na Afghanistan. Soma Taliban: Muda wa majeshi kuondoka Afghanistan hautaongezwa

Kwa mujibu wa waraka wa Marekani kuhusu mkutano huo, Marekani na Singapore zimefikia makubaliano yanayohakikisha uwepo wa Marekani katika ukanda huo kupitia mpango wa kijeshi.

 

Vyanzo: AP/Reuters