1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Marais na viongozi ECCAS wakutana Kinshasa

Jean-Noel25 Julai 2022

Wakuu wa nchi wa Jumuiya ya Kiuchumi ya Afrika ya Kati ECCAS na viongozi wengine, wanakutana mjini Kinshasa nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo,leo katika mkutano 21 utaojadili ajenda mbalimbali ikiwemo usalama

https://p.dw.com/p/4Eb1W
Felix Tshisekedi | Präsident Demokratische Republik Konogo
Picha: Arsene Mpiana/AFP/Getty Images

 

Huko mjini Kinshasa, nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, leo unafanyika mkutano wa 21 wa maraïs pamoja na viongozi wa serikali za Jumuiya ya Kiuchumi ya Afrika ya Kati (ECCAS)

Kikao hicho kinalenga kuhakikisha utendajikazi wa taasisi za jumuiya kupitia udhibiti na ufuatiliaji wa utekelezaji wa sera, pamoja na hatua zilizoidhinishwa na mamlaka ya jumuiya.

Kazi za kikao hicho zinawakutanisha hapa Kinshasa, baadhi ya maraïs na mawaziri wakuu, pamoja na maafisa wengine kutoka nchi kumi na mbili zinazounda Jumuiya ya Kiuchumi ya Afrika ya Kati.

Soma zaidi:DRC yashutumu jumuia ya kimataifa suala la amani

Maraïs ambao tayari wamewasili hapa mjini Kinshasa ni Mahamat Idriss Deby kutoka Chad, Carlos Villa Nova wa Sao Tome na Principe, pamoja na Faustin Archange Tuadéra wa Jamhuri ya Afrika ya Kati.

Ajenda ya mkutano inahusu masuala mbalimbali ya Kiuchumi, kisiasa na usalama ambayo yatatiliwa mkazo zaidi, alisema  Tina Salama, naibu msemaji wa Rais Félix Tshisekedi.

"Mda kubwa utatolewa kwa masuala ya hali ya ulinzi na usalama kufuatana na matukio ya sasa." Alisema naibu huyo msemaji wa rais Tshisekedi.

Aliongeza kwamba  wakongomaniwanapaswa kufahamu kwamba kikao hiki  kitazungumzia sana kuongezeka  mvutano baina ya Kongo na Rwanda.

"Kuna maswali mengine muhimu yatakayogusiwa, haswa kupanda kwa bei za bidhaa kwa mfano." Alisisitiza katika suala la kupanda gharama za masiha kunakoshuhudiwa kupanda kwa kasi siku hadi siku.

Masuala ya usalama yatapewa kipaumbele

Mkutano huu wa kilele unatilia mkazo usalama katika eneo hili, wakati Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo inajiandaa kupokea katika eneo lake la mashariki, kikosi cha Afrika ya Mashariki cha kupambana na makundi yanayomiliki silaha.

DR Kongo M23-Rebellen,
Askari jeshi wakiwa katika jukumu la kulinda usalama DRCPicha: Joseph Kay/AP Photo/picture alliance

Makundi hayo ambayo yanavyovuruga usalama kwenye upande huo, huhususan kundi la waasi la M23 ambao Kinshasa inalitaja kuwa ni kundi la kigaidi linaloungwa mkono na Rwanda.

Christophe Lutundula ni Naibu Waziri Mkuu anaeshughulikia masula ya Mambo ya Nje, ameweka wazi kwamba kikosi hicho ni cha kushambulia ila sicho cha kuingilia kati.

Soma zaidi:Baadhi ya makundi DRC yapinga kikosi cha jeshi la Afrika Mashariki

"Yaani jaribio za kisiasa zikishindwa ni kikosi hicho ndicho lazima kiondoe makundi yote yanayomiliki silaha, hasa M23 na wengine.

Aliongeza kwamba kwa kusema kuwa kinachohitajika sasa si kuunda kikosi kingine bali ni kikosi cha eneo kuanza kazi haraka kwa dhima ya kusambaratisha makundi yanayomiliki silaha katika taifa hilo lenye utajiri mkuibwa wa maliasili ikiwemo madini na hata misitu.

Chad, Jamhuri ya Afrika ya Kati pamoja na Sao Tome na Principe, zikiwakilishwa na marais wao kwenye mkutano huo unaoongozwa na Rais Félix Tshisekedi, nchi nyingine zinawakilishwa na mawaziri wao hasa wale wa mambo ya nje, huku Rwanda ikiwakilishwa na balozi wake hapa Kinshasa.

Tukumbuke kwamba Jumuiya ya Kiuchumi ya Afrika ya Kati iliundwa mwaka 1983 huko Libreville. Na leo inazijumuisha Gabon, Angola, Burundi, Cameroon, Kongo-Brazzaville, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Equatorial Guinea, Rwanda, Burundi, Jamhuri ya Afrika ya Kati, Sao Tome na Principe pamoja na  Chad.

Wakaazi Kivu washinikiza kuondolewa MONUSCO DRC