Maoni ya wahariri juu ya serikali mpya na juu ya Willy Brandt | Magazetini | DW | 18.12.2013
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Magazetini

Maoni ya wahariri juu ya serikali mpya na juu ya Willy Brandt

Wahariri wanatoa maoni juu ya serikali mpya ya nchini Ujerumani na juu ya Kansela wa zamani, Willy Brandt ambaeo leo angelitimiza miaka 100 laiti angelikuwa hai.

Aliekuwa Kansela wa Ujerumani Willy Brandt

Aliekuwa Kansela wa Ujerumani Willy Brandt

Gazeti la "Westdeutsche" linaanza kwa maoni juu ya serikali mpya ya mseto iliyoundwa nchini Ujerumani. Mhariri wa gazeti hilo anasema serikali hiyo inasuburiwa na changamoto kubwa , kama vile kuzeeka kwa jamii,kuhakikisha haki za kijamii sambamba na kuyashughulikia masuala ya Umoja wa Ulaya. Ili kuweza kuyashuhghulikia masuala hayo ,serikali ya mseto wa vyama vikuu inahitajika.

Gazeti la "Rhein" linauliza jee "tunaweza kuiamini serikali mpya iliyoundwa hasa kutokana na vyama vya CDU na SPD?

Mhariri wa gazeti hilo anaeleza kwamba Ujerumani haiwezi kuongozwa na kujengwa katika msingi wa mashaka. Katika kipindi cha miaka minne ya muhula wa serikali iliyoundwa,maamuzi muhimu yatafanyika ambayo hatuwezi kuyapima leo. Hata hivyo tunapaswa kuiamini serikali hiyo na tuone itakachoweza kukifanya.

Kansela Merkel

Gazeti la "Main Post" linamzungumzia Kansela Merkel aliyechaguliwa kuiongoza Ujerumani kwa mara ya tatu. Mhariri wa gazeti hilo anasema Kansela Angela Merkel ni mwanasiasa wa chama cha CDU anaezitekeleza siasa za chama cha Social Demokratik. Ndiyo kusema serikali ya mseto iliyoundwa baina ya chama chake na chama cha SPD inampoza roho. Merkel inaziwakilisha siasa za Social Demokratik vizuri sana. Na hicho ndicho hasa wanachokitaka watu nchini Ujerumani.

Willy Brandt
Aliekuwa Kansela wa Ujerumani Willy Brandt leo angelitimiza miaka100 laiti angelikuwa hai. Willy Brandt anakumbukwa sana nchini Ujerumani.Mhariri wa gaezeti la "Die Welt" anamkumbuka Kansela huyo wa zamani kwa kusema kwamba hakuna mwanasiasa wa Ujerumani alieonyesha mihemko kama Willy Brandt.

Kansela huyo wa zamani aliwagawanya wa Wajerumani katika kiwango sawa na alivyowaleta pamoja. Ndiyo sababu alichukiwa na alipendwa. Lakini ni mwanasiasa alieheshimika. Willy Brandt ataendelea kuwamo katika kumbukumbu za watu nchini Ujerumani.

Naye mhariri wa gazeti la "Die Rheinpfalz"anasema Willy Brandt hakuwa mtakatifu, kisiasa wala katika maisha yake ya faragha .Alipanda na kushuka katika maisha,yake, lakini jambo moja linapaswa kutiliwa maanani. Brandt aliuwakilisha upande mzuri wa Ujerumani duniani kote.

Na mhariri wa gazeti la "Die Glocke" anasema katika kumtathmini Willy Brandt, itakuwa sahihi kabisa kusema kwamba yeye alikuwa binadamu wa kawaida. Alikuwa na matatizo katika maisha yake ya faragha ikiwa pamoja na tatizo la ulevi-apiyapiga maji sana. Lakini alikuwa mwanasiasa mwadilifu ,alieweza kuaminika katika kutekeleza siasa zilizolenga shabaha sahihi. Mapema katika ujana wake Brandt alikuwa mpinga ufashisti.Na alipokuwa Kansela alileta mabadiliko kwa manufaa ya Ujerumani.

Mwandishi:Mtullya Abdu.Deutsche Zeitungen.

Mhariri:Mohammed Abdul-Rahman