1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Maoni: Wakati wa ujasiri wa Merkel

18 Februari 2019

Nani anaweza kuunganisha mfumo wa ulimwengu ulioparaganyika? kuhusu swali hilo Kansela wa Ujerumani Angela Merkel alitoa majibu wakati wa mkutano juu ya usalama wa mjini Munich, lakini inaonekana siyo kamili.

https://p.dw.com/p/3DbPb
MSC München Angela Merkel
Picha: Imago/photothek/F. Gärtner

Kama ilivyo kawaida ya hotuba kubwa za kisiasa, ilikuja katika muda ambao ulikua unasubiliwa. Angela Merkel alitoa hotuba ya aina hiyo katika mkutano wa usalama wa Munich.

Kwa yeyote atakayesoma hotuba yake ataweza kuelewa kwanini kulikua na msisimuko mkubwa pamoja na makofi mengi, ambayo kwa mara nyingi hufanyiwa wasanii.

Kansela wa Ujerumani Angela Merkel alizungumza bila kusoma hotuba yake, kitu ambacho hafanyi mara nyingi, na alizungumza akiwa huru. Alionyesha mfumo wa dunia hauwezi kuendelea hivi.

Alichanganua mfumo huo akizunguka dunia nzima kutoka Urusi mpaka China na kufikia mpaka Marekani, huku akirudi Ujerumani na barani Ulaya.

Alizungumzia sera zote zenye umuhimu katika siasa za kimataifa mfano sera za biashara, usalama na mazingira.

Ujumbe muafaka kwa marafiki na maadui

MSC München Angela Merkel
Picha: Reuters/A. Gebert

Hakuna kilichokua kipya katika mawazo ya Merkel, kila kitu kilishazungumzwa na kuandikwa huko nyuma, kama inavyofahamika katika juhudi zake za kujihusisha katika mahusiano ya kimataifa ya pande nyingi. Sasa ameamua kusema kila kitu kama kilivyo.

Maneno yake yalikua ni kama ushindi kwa wasikilizaji hasa wale waliotofautiana sana na hotuba ya makamu wa Rais wa Marekani, Mike Pence. 

Bi Merkel alizungumza  kwa ucheshi huku akijikosoa kwa mapungufu ya sera ya nje ya Ujerumani. Kwa upande mwengine, Mike Pence, aliwaonyesha wasikilizaji jinsi sera ya Marekani kwanza inamaanisha nini kiuhalisia. Utofauti kati ya hizo hotuba mbili ulionyesha kuwa mahusiano kati ya Ulaya na Amerika ya Kaskazini yalivyo katika wakati mbaya.

Mrithi wake anajiandaa kwa Uchaguzi

Huku uungwaji wake mkono nyumbani ukitetereka lakini kwa kimataifa ukiongezeka, Merkel ni kama makansela wengine waliopita mfano Konrad Adenauer, Willy Brandt, Helmut Schmidt na Helmut Kohl.

Wote umaarufu wao nyumbani ulipungua hadi kusababisha  wengine kutolewa kwenye nafasi zao, wakati umaarufu wao duniani kote ulikuwa ukiongezeka.

Bundeskanzlerin Angela Merkel bei der Münchner Sicherheitskonferenz 2019
Picha: DW/M. Drabok

Angela Merkel ameshampa uongozi wa chama cha CDU kwa Annegret Kramp-Karrenbauer. Alitumia mkutano huo wa Munich wa ulinzi katika kujitambulisha katika mitandao ya wana sera za nje, zitakazomwezesha kushiriki mikutano mbali mbali hapo baadaye.

Mrithi wake alishazungumza pia katika mahojiano juu ya mwelekeo wake wa sera za nje na sasa anajipanga vizuri kwa hilo.

Juu ya nani atatupeleka kwenye dunia yenye utulivu, Merkel anaamini kwamba wote tunajukumu hilo na inabidi tusaidiane katika hilo. Ingawa yeye hatoshiriki tena katika vikao vya huko baadaye kama Kansela, lakini urithi wake kwenye upande wa sera za mambo ya nje zimejionyesha katika mkutano wa usalama wa Munich.

Mwandishi: Trippe, Christian

Mtafsiri: Harrison Mwilima

Mhariri: Daniel Gakuba