Manchester United na Inter Milan leo | Michezo | DW | 24.02.2009
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Michezo

Manchester United na Inter Milan leo

duru ya timu 16 za kombe la Ulaya.

default

Mabingwa Manu wakishangiria taji lao.

Baada ya likizo ya x-masi na mwaka mpya,kinyangannyiro cha champions league-kombe la klabu bingwa barani ulaya, kinarudi uwanjani leo na kesho .

Mabingwa wa kombe hilo Manchester United ya Uingereza, wana kibarua kigumu jioni hii huko Milan,Itali kuwapiga kumbo wenyeji wao Inter Milan.Kesho, itakua zamu ya mabingwa wa Ujerumani Bayern Munich, walioteleza mara tatu mwaka huu katika Bundesliga wakiwa na miadi na FC Porto ya Ureno.

Katika changamoto za jioni hii,mabingwa wa dunia,ulaya na Uingereza Manchester United ,wanabidi kutamba dhidi ya timu ya kocha mreno Jose Mouirinho-Inter Milan,mabingwa wa Itali.Mourinho mtakumbuka ,alikua kocha wa Chelsea na analielewa dimba la Uingereza na hasa Manu.Isitoshe, ni yeye alieongoza FC Porto ya Ureno 2004 kutwaa kombe hili la ulaya.Kwahivyo, Sir Alex Ferguson anajua anawaongoza akina Cristiano Ronaldo katika pori la simba mjini Milan.

Vita vya dimba kati ya waingereza na wataliana, vinaendelezwa na kutimizwa kwa miadi nyengine kati ya AS Roma na Arsenal mjini London.Arsenal imemudu suluhu tu mechi zake 3 ziliozopita za champions League na hiyo si dalili njema.

Atletico Madrid pia wako uwanjani leo wakiwakaribisha nyumbani FC Porto,mabingwa wa 2004.

Viongozi wa La Liga-ligi ya Spain -FC Barcelona,wamepata pigo kali mwishoni mwa wiki walipozabwa mabao 2-1 na Espanyol iliopo mkian;na simba wao wa nyika -mkamerun Samuel Eto-o atabidi leo kunguruma kweli kuiokoa Barcelona isizikwe katika kaburi waliochimbiwa tayari na Olympique Lyon.

Kesho mabingwa wa Ujerumani bayern munich walikionas cha mtema kuni jumamosi mbele ya FC Cologne,wana miadi na Sporting Lisbon ya ureno wakitumai jogoo lao linalougua mtaliana Luca Toni litakua limepona kuwaepusha na wembe ul,iowanyoa nyumbani jumamosi usije ukawanyoa tena ugenini Lisbon.

Munich imeshindwa mapambano yake 3 yaliopita nyumbani katika Bundesliga na Luca toni alichechemea baada ya kuumia katika mpambano wa wiki ya nyuma dhidi ya Hertha Berlin.

Real madrid inakutana kesho pia na FC Liverpool wakati Chelsea ikitamba tena na Muivory Coast Didier Drogba na mfaransa Nicolas Anelka inaonana na Juventus ya Itali.

Matangazo

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com