Manchester United kupambana na B.Munich Champ-League | Michezo | DW | 19.03.2010
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Michezo

Manchester United kupambana na B.Munich Champ-League

TP Mazembe yakaribishwa Kigali kutetea taji lake.

Chipukizi wa Bayern Munich atamba David Alaba.

Chipukizi wa Bayern Munich atamba David Alaba.

TP Mazembe, mabingwa watetezi wa Kombe la klabu bingwa barani Afrika kutoka Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo na mabingwa mara 6 wa Kombe hilo, Al Ahly ya Misri, ni miongoni mwa timu zinazoingia uwanjani mwishoni mwa wiki hii kwa msimu mpya .Kombe la Dunia la chipukizi wa mitaani-street kids, laanza nchini Afrika kusini, Timu ya chipikuzi ya Tanzania itarudi na kombe ?

Katika ringi ya mabondia, mbabe wa wezani wa juu ulimwenguni, Muukraine Wladmir Klitschko,adai adui yake leo usiku (Jumamosi) Muamerika, Eddie Chambers, hataondoka Ujerumani na taji la WBO na la IBF.

Felix Magath, kocha alieitawaza Wolfsburg msimu uliopita mabingwa wa Bundesliga na sasa kocha wa Schalke 04, anarudi Hamburg, klabu yake ya zamani kwa mpambano wa kesho Jumapili wa Bundesliga. Hamburg iko nafasi ya 5 ya ngazi ya ligi na imekata juzi tiketi yake ya robo-finali ya Kombe la Ligi la Ulaya, licha kulazwa na Anderlecht ya Ubelgiji.Bayern Munich, ambayo wiki ijayo itakua na miadi na Bayer Leverkusen,

timu 2 ziliopo kileleni, leo inapigania pointi 3 huko Frankfurt. Werder Bremen, iliotimuliwa juzi nje ya Kombe la ligi la Ulaya na Valencia ya Spain, licha ya kumalizana sare mabao 4:4, leo inanawakarimu nyumbani mwao Bochum, wakati Stuttgart ilioaga kombe la (champions league ) la Ulaya hapo juzi, baada ya Lionel Messi wa FC BARCELONA kuichezesha kindumbwe-ndumbwe na kuwatoa kwa mabao 3:0, inapambana jioni hii na Hannover. Hannover inatamani jioni hii ushindi tena kufa- kupona ili kujikomboa kutoka safu ya timu 3 zinazoweza kuteremshwa daraja ya pili.

Bayer Leverkusen, ina kibarua kigumu kuondoka na pointi zote 3 jioni hii kutoka Borussia Dortmund. Leverkusen haikuwahi kutwaa ubingwa wa Ujerumani, lakini msimu huu yawezekana tena, mradi wasiteleze tena.

Mabingwa Wolfsburg, ambao wamewika katika kombe la Ligi la ulaya juzi kwa kuitoa Rubin Kazan ya Moscow 2:1 , ina miadi kesho na Hertha Berlin.Duru ya mwishoni mwa wiki hii, ilianza jana kwa changamoto kati ya mahasimu 2 wa jadi: FC Cologne na Borussia Moenchengladbach chini ya ulinzi mkali wa polisi. Kila timu haikudiriki kushindwa.

Liverpool, inajiwinda kutoa changamoto kesho (Jumapili) kwa Manchester united. Ushindi wa Liverpool wa mabao 4-1 dhidi ya Portsmouth,Jumatatu iliopita, unabainisha jinsi Liverpool ilivyo rudi kutamba. Na salamu hizo, bila shaka, Manu imezipata.

Arsenal iliopo pointi 2 nyuma ya Manu, yaweza kuparamia kileleni mwa ngazi ya Premier League leo, kwa vile, inatamba nyumbani mbele ya West Ham inayopepesuka kuteremshwa daraja ya pili. Chelsea, iliokiona cha mtemakuni ilipopigwa kumbo na Inter Milan nje ya Champions League majuzi, ikiwa pointi sawa na Arsenaal imefunga safari kuitembelea Blackburn Rovers kwa zahama yao ya hapo kesho. Stadi wao, Didier Drogba, amewataka kuongeza hamasa ya mchezo baada ya pigo la Champions League.

Mabinghwa watetezi wa Kombe la klabu bingwa barani Afrika , TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo na mabingwa mara 6 wa Kombe hilo, Al Ahly ya Misri, wanarudi uwanjani leo na kesho kuania taji hilo:

Mazembe ambayo mwaka jana walitwaa kombe hilo kwa mara ya 3 baada ya kupita kitambo cha miaka 49, wana vita na Jeshi la Rwanda APR tena mjini Kigali. Al Ahly, wanakaribishwa nyumbani mwa Gunners ya Zimbabwe.

Usiku wa leo (Jumamosi) , wababe wawili wa wezani wa juu ulimwenguni watazichapa ndondi ringini mjini Düsseldorf, Ujerumani: Bingwa wa dunia wa wezani wa juu, Muukraine Wladmir Klitschko, anaingia ringini kuzima changamoto za Eddie Chambers wa Marekani, akimuahidi Chambers kuwa hataondoka Dusseldorf na taji lake la WBO na IBF. Huu ni mpambano wa 17 wa Klitchko wa kutetea taji lake .

Mwandishi: Ramadhan Ali /DPAE/AFPE

Uhariri: Miraji Othman