1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Nani mshindi kati ya Manchester City na Inter Milan ?

10 Juni 2023

Timu ya Manchester City itamenyana leo na Inter Milan kwenye fainali ya Ligi ya Mabingwa, FA katika uwanja wa Ataturk Olympic mjini Istanbul, Uturuki.

https://p.dw.com/p/4SPro
 Premier League Fussball l Manchester City vs West Ham United l Erling Haaland
Picha: Martin Rickett/empics/picture alliance

Manchester City itateremka dimbani Ataturk Olympic mjini Istanbul leo usiku kujaribu kushinda Ligi ya Mabingwa kwa mara ya kwanza na hatimaye kushinda mataji matatu msimu huu watakapocheza dhidi ya Inter Milan katika mechi ya fainali.

Vijana wa Pep Guardiola tayari wameshinda taji la Ligi Kuu ya Premia na Kombe la FA.

Hii ni mara ya pili katika kipindi cha miaka mitatu kwa Manchester City kufika fainali ya Ligi ya Mabingwa barani Ulaya, na walifungwa na Chelsea msimu wa mwaka 2020-21.

Guardiola anasaka taji lake la Ulaya kwa mara ya kwanza tangu alipofanya hivyo mnamo mwaka 2011 akiwa mkufunzi wa Barcelona, ambapo pia alishinda mataji matatu miaka miwili kabla ya hapo.

Manchester United ndio klabu pekee ya Uingereza iliyowahi kushinda mataji matatu kwa msimu mmoja. Mnamo mwaka 1999, Mashetani hao wekundu walishinda taji la Ligi Kuu ya Premia, Kombe la FA na Ligi ya Mabingwa barani Ulaya.

Inter Milan haijapewa nafasi kubwa ya kushinda mechi ya leo, japo ina historia nzuri ya Ulaya tofauti na City, kwani wamewahi kushinda Ligi ya mabingwa barani Ulaya mara tatu. Mara ya mwisho kushinda taji hilo ilikuwa mnamo mwaka 2010, wakati huo ikitiwa makali na Jose Mourinho.