1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroMamlaka ya Palestina

Malori ya misaada kutoka Misri yaanza kuingia Gaza

26 Mei 2024

Malori yaliyobeba misaada kutoka Misri yameanza kuingia ndani ya ukanda wa Gaza kupitia kivuko kinachodhibitiwa na Israel cha Kerem Shalom.

https://p.dw.com/p/4gI6k
Shehena ya misaada inayotarajiwa kwenda Gaza ikikaguliwa katika kivuko cha Kerem Shalom
Shehena ya misaada inayotarajiwa kwenda Gaza ikikaguliwa katika kivuko cha Kerem ShalomPicha: Jack Guez/AFP/Getty Images

Shirika la habari la Misri la Al-Qahera limeripoti kuwa jumla ya malori 200 yameondoka kutoka upande wa Misri wa kivuko cha Rafah ambacho kimefungwa tangu mapema mwezi Mei baada ya jeshi la Israel kuchukua udhibiti wa eneo hilo upande wa Palestina.

Al-Qahera hata hivyo halikuweka wazi idadi ya malori yaliyofanikiwa kufanyiwa ukaguzi na kuingia Gaza, japo limeripoti kuwa tayari malori manne ya kubeba mafuta yameingia Gaza na sasa yanaelekea hospitali.

Soma pia: Mapigano yanaendelea katika mji wa kusini mwa Gaza Rafah

Mkuu wa shirika la hilali nyekundu la Misri Khaled Zayed katika eneo la Al-Arish ambapo misaada mingi huwasili, ameliambia shirika la habari la AFP kuwa malori yaliyosalia yanatarajiwa kuvuka na kuingia Gaza leo.

Misaada yote kutoka Misri kwanza hukaguliwa na mamlaka ya Israel na kusambazwa kwa ushirikiano na Umoja wa Mataifa.