Sheria na HakiUrusi
Mahakama ya Urusi yawahukumu vifungo maafisa wa ICC
12 Desemba 2025
Matangazo
Mwendesha Mashtaka Mkuu wa ICC Karim Khan amehukumiwa kifungo cha miaka 15 gerezani, ambapo miaka tisa ataitumikia gerezani na iliyosalia mahali wanapoadhibiwa wahalifu wakubwa, hii ikiwa ni kulingana na Ofisi ya Mwendesha Mashtaka Mkuu wa Urusi hii leo.
Majaji wanane wa ICC iliyoko mjini The Hague pia wamehukumiwa vifungo vya kati ya miaka mitatu na nusu hadi 15 jela.
Kulingana na Urusi, Khan alifungua kesi haramu za uhalifu dhidi ya raia wa taifa hilo kuanzia mwezi Februari hadi Machi, 2022 na kupelekea kutolewa kwa waranti usio halali wa kumkamata Rais Vladimir Putin, miongoni mwa viongozi wengine.
Hata hivyo, hukumu hiyo haitakuwa na matokeo kwa sasa kwa kuwa Khan hayuko Urusi.