1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
Sheria na HakiAfrika

Mahakama Italia yaharamisha kuwarejesha wahamiaji Libya

19 Februari 2024

Mahakama ya ngazi za juu ya rufaa nchini Italia imesema kuwarejesha nchini Libya wahamiaji wanaoingia nchini humo wakipitia baharini ni kinyume cha sheria, uamuzi uliopongezwa na mashirika ya misaada na haki za binadamu.

https://p.dw.com/p/4cYyB
Wahamiaji
Baadhi ya wahamiajiPicha: Franziska Wüst/DW

Mahakama hiyo imeidhinisha hukumu ya nahodha wa mashua ya uokozi ya Italia, aliyefahamika kwa jina moja la Asso mwenye umri wa miaka 28, ambaye mwaka 2018 aliwaokoa wahamiaji 101 na kuwarejesha nchini Libya.  Wanawake wajawazito na watoto walikuwa miongoni mwa watu hao.

Soma pia:Wahamiaji 80 wameokolewa, wawili wafa pwani ya Libya

Nahodha huyo alihukumiwa kifungo cha mwaka mmoja jela kwa kuwatelekeza watu waliokuwa katika uhitaji, ikiwa ni pamoja na watoto wadogo.

Hata hivyo, uwezekano ni mdogo kwa nahodha huyo kwenda jela, kwa kuwa nchini Italia hukumu iliyo chini ya miaka minne, si lazima kutekelezwa gerezani.