1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Magazetini: Merkel ziarani katika bara la Afrika

Sekione Kitojo
30 Agosti 2018

Wahariri wa magazeti ya Ujerumani wamejishughulisha zaidi na mada kuhusu ziara ya kansela Angela Merkel barani Afrika, Ujerumani kurejesha mafuvu ya watu waliouwawa katika enzi za ukoloni wa Ujerumani nchini Namibia.

https://p.dw.com/p/342BM
Republik Senegal - Kanzlerin Merkel besucht Senegal
Kansela wa Ujerumani Angela Merkel akiwa na rais wa Senegal Macky SallPicha: picture-alliance/dpa/M. Kappeler

Tukianza  na  gazeti la  Markische Oderzeitung  la  mjini Ftrankfurt , mhariri  anaadika  kwamba  kansela  anafanya ziara  nchini  Senegal, Ghana  na  Nigeria. Mhariri anaendelea:

"Wakati  huo  huo  waziri  wa  ushirikiano  wa  maendeleo Gerd Mueller  anafanya  ziara   katika  mataifa  mengine  ya Afrika. Bila  shaka,  Ujerumani  imekuwa  wakati  wote ikilitupia  jicho   bara  la  Afrika. Katika  kupambana  na masuala  ya  wakimbizi, kuhusu mahitaji  ya  maendeleo na uwezekano  wa  uwekezaji hususan  kwa  makampuni  ya Ujerumani.  Haya  yote  ni  mambo  mazuri  na  sahihi. Bora zaidi  lakini , ingekuwa  sahihi, iwapo  kungekuwa  na mkakati  maalum  wa  utendaji  wa  hayo  yote.  Kwa  kuwa hilo  bado  halieleweki."

Kuhusiana  na  mada  ya  enzi  za utawala  wa  kikoloni nchini  Namibia , mhariri  wa  gazeti  la  Nuernberger Nachrichten , anaandika  kwamba, vinyago ,  mapambo  na vifaa  vya  sanaa  kutoka  katika  mataifa  ya  Afrika mara nyingi  sio  kwamba  vimekuwapo tu  katika  majumba  ya makumbusho  ya  Ulaya, lakini  kwa  kiasi  kikubwa vinafungamanishwa  na  historia  ya  ukoloni. Mhariri anaandika:

"Na  mara  nyingi  ni  kama uporaji  wa  sanaa. Na historia ya  ukoloni  wa  Ujerumani  kwa  kweli  si  ya  muda  mrefu , ilidumu si  zaidi  ya  miongo  mitatu  na  kumalizika  mwaka 1918 kwa  kushindwa  kwa  Ujerumani  katika  vita  vikuu vya  kwanza  vya  dunia. Matokeo  yake  lakini yanaonekana  hadi  hii  leo. Mada  hii lakini inapaswa kuangaliwa kwa undani  kwa  kuwa Ujerumani ni  nchi ambayo ina  wahamiaji  wengi hivi  sasa. Watu  kutoka bara  la  Afrika  ama  mashariki  ya  kati   hivi  karibuni  ama baadaye watatuuliza  maswali  kuhusu  urithi  wao  wa kiutamaduni. Hii  haihusiani  na  suala  la  kurejesha  vitu vyote vilivyokusanywa  kutoka  katika  enzi  za  ukoloni. Lakini  ni  lazima  kuwe  na  mjadala  wenye  usawa pamoja na  mataifa  haya  ambayo sanaa  hizi zimechukuliwa, kuhusu  nini  kilitokea  wakati  wa  uporaji wa  urithi  huu  wa  utamaduni."

Mhariri  wa  gazeti  la  Hessische Niedersaechsische Allgemeine la  mjini  Kassel , akizungumzia  kuhusu  mada hiyo  ya enzi  za  utawala  wa  kikoloni  wa  Ujerumani nchini  Namibia  anaandika:

"Hatua  nyingine  ni  lazima ichukuliwe.  Ni  lazima  kuomba rasmi  samahani  ambayo  hadi  sasa  bado  suala  hilo halijafanyika. Ni enzi  za  aibu. Haitakuwa  vizuri  kwa kuchukua  hatua  nzuri  tu. Serikali  ya  Ujerumani  haioni sababu  yoyote  ya  msingi  kwa madai ya  Namibia  ya kupatiwa  fidia  ama  kwa  watu  mmoja  mmoja wa  kabila la  Herero  na Wanama. Lakini  kuna  ulazima  wa  takriban kufikiwa  makubaliano  juu ya  kupatiwa  msaada  makabila hayo  mawili."

Kuhusiana  na  mada  juu  ya  tathmini  ya  kocha  wa  timu ya  taifa  ya  Ujerumani Joachim Loew kwa  kutolewa  na mapema  timu  ya  taifa  katika  fainlai  za  kombe  la  dunia nchini  Urusi  mwaka  huu, mhariri  wa  gazeti  la Mitteldeutsche Zeitung  la  mjini  Halle  anaandika:

"Kutokana  na  matatizo  mengi , wakati wa  fainali  za kombe  la  dunia  na katika  timu  ya  taifa , ni  wazi kwamba  mambo  haya  yanatofautiana, na kwamba  kocha Loew  pamoja  na  mkurugenzi  wake  wa  soka  Oliver Bierhof wameyaelewa  kidogo  ama hawajayaelewa kabisa. Hilo limeonekana  katika  tathmini. Huo si mwanzo  mpya, badala  yake ni  ushuhuda wa kushindwa."

 

Mwandishi:   Sekione  Kitojo / ilandspresse

Mahriri: Mohammed Khelef