1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Maelfu ya wakulima waandamana India

Saumu Mwasimba
21 Februari 2024

Maelfu ya wakulima India wamendamana na kreni na tingatinga wanajiandaa kuingia kwenye mji mkuu wa nchi hiyo New Delhi.

https://p.dw.com/p/4cfux
Polisi wakiweka kizuizi kuwazuia wakulima wanaondamana kuelekea New Delhi
Polisi wakiweka kizuizi kuwazuia wakulima wanaondamana kuelekea New DelhiPicha: Adnan Abidi/REUTERS

Maandamano hayo yanatokea baada ya mazungumzo na serikali kushindwa kutimiza madai yao ya kutaka kuhakikishiwa viwango vya bei vya kuuza mazao yao.

Askari wa kulinda usalama waliojihami kwa vifaa vya kukabiliana na vurugu, wako kufuatilia maandamano hayo.

Wakulima hao wengi wakitokea mkoa wa Kaskazini mwa India wa Punjab wamekuwa wakiitaka serikali kupitisha sheria ya kuongeza  bei mazao wanayozalisha.

Wakulima hao ni kundi kubwa lenye ushawishi la wapiga kura ambao Waziri Mkuu Narendra Modi hatoweza kulikasirisha katika wakati nchi hiyo inaelekea kwenye uchaguzi mkuu mwezi Mei.