Macron atuma ujumbe kwa Trump kutaka kuandaa mkutano wa G7
20 Januari 2026
Matangazo
Macron amesema Ukraine, Urusi, Denmark na Syria pia zinaweza kualikiwa pembezoni mwa mkutano huo.
Haya yamethibitishwa na vyanzo vya karibu na rais huyo.
Katika ujumbe huo, Macron amemwambia Trump kwamba wako pamoja katika suala la Syria na kwamba wanaweza kufanya mambo makubwa nchini Iran.
Ameongeza kusema haelewi anachokifanya Trump kuhusu kisiwa cha Greenland.
Trump pia alichapisha ujumbe huu kwenye mtandao wake wa kijamii wa Truth.
Uhusiano wa Trump na Macron ulizidi kudidimia jana wakati rais huyo wa Marekani alipotishia kutoza asilimia 200 ya ushuru kwa mvinyo wa Ufaransa kutokana na nia ya nchi hiyo ya kukataa mwaliko wa kujiunga na "Bodi yake ya Amani".