1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
Migogoro

Macron asema vikosi vya usalam vitasalia New Caledonia

23 Mei 2024

Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron amesema leo kuwa vikosi vya usalama vitasalia katika eneo lililokumbwa na vurugu la New Caledonia kadiri itakavyohitajika.

https://p.dw.com/p/4gAUv
New Caledonia| Emmanuel Macron
Macron amekwenda New Caledonia kufanya mazungumzo y akutuliza haliPicha: Ludovic Marin/Pool Photo via AP/picture alliance

Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron amesema leo kuwa vikosi vya usalama vitasalia katika eneo lililokumbwa na vurugu la New Caledonia kadiri itakavyohitajika, na kuongeza kuwa hali ya dharura iliyotangazwa katika kisiwa hicho cha pasifiki haipaswi kurefusha.

Macron aliwasili New Caledonia leo Alhamisi kwa ajili ya mazungumzo ya siku moja, ambapo atalenga kubadili ukurasa kufuatia mandamano ya vurugu yaliosababishwa na mabadiliko ya kisheria ya uchaguzi yaliopingwa na wenyeji wa kisiwa hicho kinachotawaliwa bado na Ufaransa.

Soma pia: Ufaransa yapeleka wanajeshi New Caledonia kuzima ghasia

Watu sita wameuawa katika machafuko yalioachwa maduka yakiwa yameporwa, na magari na mabasi kuchomwa moto. Serikali ya Ufaransa imetuma mamia ya polisi wa ziada kusaidi kurejesha utulivu.

Rais Macron amesema askari wa ziara wapatao 3,000 watasalia huko hata wakati wa mashindano ya olimpki ya Paris, ikiwa itahitajika.