1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaUfaransa

Macron asema mazungumzo zaidi kufanyika kuhusu New Caledonia

23 Mei 2024

Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron ameahidi leo kutolazimisha mageuzi ya marekebisho ya sheria za uchaguzi katika eneo la New Caledonia ambayo yamesababisha ghasia mbaya, na kusema kuwa mazungumzo zaidi yanahitajika.

https://p.dw.com/p/4gDJG
Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron
Rais wa Ufaransa Emmanuel MacronPicha: Ludovic Marin/AP Photo/picture alliance

Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron ameahidi leo kutolazimisha mageuzi ya marekebisho ya sheria za uchaguzi katika eneo la New Caledonia ambayo yamesababisha ghasia mbaya, na kusema kuwa mazungumzo zaidi yanahitajika.

Macron amewaambia wanahabari katika eneo hilo kwamba ameahidi mageuzi hayo hayatapitishwa sasa katika muktadha ulioko.

Soma pia: Macron asema vikosi vya usalam vitasalia New Caledonia

Rais huyo ameongeza kusema, "Tunahitaji kuangalia taswira nzima, na kuona jinsi gani tunaweza kupata kile ninachoweza kuita 'utulivu wa manufaa'. Kwa maneno mengine, kurejesha utulivu, uwezo wa kufanya mazungumzo na kupata suluhisho. Lakini kutuliza hali hakuwezi kumaanisha kurudi nyuma. Kutuliza hali hakuwezi kumaanisha kutoheshimu maoni ya wengi ambayo tayari yamefanyika."

Macron amesema wataruhusu wiki kadhaa za kurejesha utulivu na kuanza tena kwa mazungumzo ili kupata maelewano mapana miongoni mwa pande zote na kutathmini tena hali hiyo ndani ya mwezi mmoja.