1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Maandamano makubwa DDR ya Novemba 4, 1989

Sekione Kitojo
4 Novemba 2019

Tarehe 4 Novemba mwaka  1989 ni siku inayokumbukwa  nchini Ujerumani  kutokana  na  kuanza  maandamano  makubwa  katika historia  ya  iliyokuwa  Ujerumani  mashariki yaani DDR.

https://p.dw.com/p/3SQ6e
Deutschland Alexanderplatz-Demonstration 1989
Maandamano ya Alexanderpatz mjini Berlin mwaka 1989Picha: picture-alliance/dpa

Maelfu  kadhaa ya  wapinzani  walidai wakati  huo  pamoja  na  wawakilishi  wa  serikali kuwapo  na  mageuzi ya  kisiasa. Hata  hivyo kitengo cha  usalama  wa taifa  maarufu  kama  Stasi  kilikuwa  kimeingiwa  na  hofu. 

Kulikuwa  tayari  na  tetesi  katika  Jamhuri ya  Kidemokrasi ya Ujerumani , DDR. Wananchi  kwa  miezi  kadhaa walikuwa  wanapima kujitoa  kutoka  katika  maficho  na  kuingia  mitaani. Mjini  Leipzig walikuwa  watu wakiandamana  kila  mwezi  kwa  ajili  ya uhuru wa kutoa  maoni  na  uhuru  wa  kusafiri wapendako. Zaidi na  zaidi wananchi  wa  nchi  hiyo  wamekuwa  wakiipa  kisogo  nchi hiyo inayofilisika  kisiasa  pamoja  na  kiuchumi. Utawala  wa  kikomunisti  wa DDR ulikuwa  ukiwaita  watu wenye  mwelekeo  huo  kuwa  ni  wakimbizi wanaoikimbia jamhuri  hiyo.

Deutschland Montagsdemonstration in Leipzig 1989
Maandamano ya kila Jumatatu mjini Leipzig mwaka 1989Picha: picture-alliance/Lehtikuva Oy/H. Saukkomaa

Erich Honecker , ambaye  kuanzia  mwaka  1973  alishika  madaraka ya  nchi  hiyo, aliondolewa  madarakani  Oktoba  18. Lakini  hata  mrithi wake Egon Krenz hakupata  uungwaji  mkono  na  wananchi  wake. Kutokana  na  hali  hii tarehe 4 Novemba  1989 yalifanyika rasmi maandamano  makubwa  yaliyopata  kibali  katika  historia  ya Ujerumani  mashariki  DDR.

Waliotayarisha ni  wacheza  sinema na  watu wanaohusika  katika maigizo  ya tamthilia  kutoka  Berlin mashariki. Walidai kuhusu  vifungu vya  katiba  27 na  28 , ambavyo  ni  uhuru  wa  kutoa  maoni,uhuru  wa vyombo  vya  habari na  uhuru  wa  kukusanyika.  Vifungu  hivi kwa muda  wa  miaka  40  ya  DDR  vilikuwapo tu kwa  nadharia.

Revolution in Osteuropa 1989 Bild 15 DDR Erich Honecker tritt zurück
Kiongozi wa DDR wakati huo Erich HoneckerPicha: AP

Katika  siku  hii  lakini  katiba  ambayo  kwa  muda  mrefu  ilikanyagwa ilirejeshewa  uhai na kundi  kubwa  la  binadamu  waliojitokeza  katika uwanja wa  Alexanderplatz  mjini  Berlin.

Makadirio yanatofautiana  miaka  30  baadae  kwamba  watu 200,000 na  milioni  moja  walishiriki  katika  maandamano  hayo.

Kiongozi wa chama tawala 

Kile  walichokishuhudia  kilikuwa ni  hali  ya  kipekee  kabisa  katika historia ya  Ujerumani mashariki. Waandamanaji  walikusanyika  mbele ya  gari  ndogo  ya  kubeba  mizigo, na  katika  eneo  dogo  la  uwazi kati  ya  maduka  kuliwekwa  jukwaa  dogo  la  mbao. Hilo lilikuwa jukwaa  lililotumiwa  na  zaidi  ya  wazungumzaji 20. Wacheza  sinema, waimbaji, watunzi wa  vitabu, na wachungaji  na  mapadre, lakini  pia wawakilishi wa  utawala.

Mmoja miongoni  mwao  alitokea  kuwa  maarufu  siku  tano  baadaye, Novemba 9 , 1989 duniani  kote. Guenter Schabowski,  mwenyekiti wa chama  tawala  mjini  Berlin cha  Sozialistishe Einheitspartei Deutschland, SED.

20 Jahre Mauerfall Momentaufnahme
Egon Krenz (kushoto) aliyeshika madaraka baada ya Erich HoneckerPicha: DW

Katika  hali  hii  alitangaza  katika  mkutano  na  waandishi  habari sheria  mpya  iliyohusu  watu  kusafiri,  hatua  ambayo  ilisababisha kwa  hali  ya  mshangao  kuja  kuanguka  kwa  ukuta  wa  Berlin. Katika maandamano  ya  tarehe 4, Novemba Schabowski  alizomewa  sana na waandamanaji.

Hata pale alipoanza  kusema , "tunaidhinisha  utamaduni wa kujadiliana".

Watendaji wa  utawala  wa  kikatili  wa  DDR katika  wakati  huu walikuwa  wamepoteza  kila  aina  ya  uaminifu. Hatua ya Schabowski ya  kujikosoa ilizimwa  na kelele za  waandamanaji.

Ukomunisti waanguka

"Ni nini  kinaweza  kuuendesha ukoministi  katika  mtazamo  huu  na mwelekeo huu wa  maelfu ya watu ?" Aliuliza kundi  hilo  kubwa  la  watu ambao  bila  shaka  walikuwa wana mtazamo wa  chuki dhidi  yake. Jibu lake  binafsi lilikuwa , "Ni yule tu anayesikia na  kuelewa  onyo, anaweza kuanza upya."

Deutschland, Brandenburger-Tor, Maueröffnung 1989
Watu wakiwa juu ya ukuta wa Berlin kabla ya kuangushwaPicha: picture-alliance/W.Kumm

Mmoja wa  watu ambao waliyachukua  maneno ya  Schabowski , alikuwa  mkosioaji  mkubwa  wa  utawala  wa  DDR Friedlich Schorlemmer. Mwanathiolojia  huyo  kutoka  Wiitenberg, mji alikozaliwa muasisi wa  mageuzi katika  kanisa la kiluteri , Martin Luther, alinukuu mabadiliko ya  wimbo  wa  taifa  wa  DDR: "Majira ya Mapukutiko mwaka 1989 tulikubaliana  kubadilisha  magofu na  kujenga upya mustakabali wetu." Kutokana  na hisia za  wakimbizi  wengi  wa  DDR aliwataka  wananchi  kubakia  katika  eneo  hilo, na  kuijenga  upya  nchi hiyo.  Hivi  sasa  tunamhitaji  kila  mmoja  wetu."

Mcheza sinema  kijana  Jan-Josef Liefers, ambae katika  Ujerumani ya sasa  iliyoungana  amekuwa  maarufu  katika  kipindi  cha  televisheni cha Tartort, aliwatupia  swali la  wazi viongozi wa  chama  cha  SED: Kwa kuwa  viongozi wa  juu  wa  SED  wanachukua  hatua kutokana  na mbinyo  kutoka  kwetu,  mtazamo wangu  ni  kwamba  jukumu  lao  la hapo zamani  halistahili tena  kuzungumzwa.

Kundi  kubwa  la  watu  katika  uwanja  wa  Alexanderpatz  lilitaka kusikia  maneno kama  hayo. 

Kulikuwa  na  shangwe  kubwa.