1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
Sheria na HakiSyria

Maafisa watatu waandamizi wa Syria wahukumiwa Ufaransa

25 Mei 2024

Mahakama moja nchini Ufaransa imewahukumu kifungo cha maisha jela maafisa watatu wa ngazi za juu wa Syria waliokutwa na hatia ya uhalifu wa kivita.

https://p.dw.com/p/4gHB5
Nembo ya Sheria
Nembo ya SheriaPicha: Damien Meyer/AFP/Getty Images

Maafisa hao ni wa ngazi za juu zaidi nchini Syria kushitakiwa kwa uhalifu dhidi ya ubinaadamu katika mahakama ya Ulaya.

Mashitaka dhidi yao yalihusisha kisa cha kupotea kwa raia wenye uraia pacha wa Syria na Ufaransa ambao ni Mazzen Dabbagh pamoja na mwanae Patrick waliokamatwa na maafisa hao, na baadae waliripotiwa kufariki wakiwa korokoroni.

Damascus- Rais wa Syria Bashar al-Assad
Rais wa Syria Bashar al-AssadPicha: via REUTERS

Kesi ya maafisa hao watatu iliendeshwa kwa siku nne wakiwa hawapo mahakamani. Miongoni mwao ni Ali Mamlouk, aliyekuwa mkuu wa Ofisi ya Usalama wa Taifa ambaye bado anahudumu kama mshauri wa usalama katika ofisi ya Rais wa Syria Bashar al-Assad.

Soma pia: Kiongozi wa zamani wa wanamgambo Syria ashitakiwa Ujerumani

Wengine ni Jamil Hassan, aliyekuwa mkurugenzi wa idara ya ujasusi kwenye jeshi la anga na Abdel Salam Mahmoud, aliyekuwa mkuu wa upelelezi.