Münich yaaibishwa na Cottbus | Michezo | DW | 17.03.2008
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Michezo

Münich yaaibishwa na Cottbus

Viongozi wa ligi ya ujerumani B.Munich wamezabwa mabao 2:0 na chipukizi E.Cottbus na Bremn imekula bao 1:0 huko Wolfsburg.

Felix Magath

Felix Magath

Katika changamoto za mwishoni mwa wiki za Bundesliga-Ligi ya Ujerumani- viongozi wa Ligi-Bayern Munich walikiona cha mtema kuni kutoka chipukzi Energie Cottbus.Bremen iliokua ikifukuzia B.Munich nafasi ya pili kileleni, ilipata pigo jengine mara hii kutoka Wolfsburg.

Barcelona imepunguza pointi 1 tu mwanya wake na Real Madrid kileleni mwa la Liga kwa kutoka sare 2:2.

►◄

Tukianza na changamoto za ligi ya Ujerumani mwishoni mwa wiki-tangu Bayern Munich inayoongoza Ligi kwa pointi 5 na WerderBremen iliokua ikifukuzia nafasi ya pili, zimeteleza tena.Wakati Munich imechapwa mabao 2-0 na timu iliopo mkiani mwa ligi Energie Cottbus, Werder Bremen imezabwa bao 1:0 na jirani yake Wolfsburg huko kaskazini.

Pigo la Bayern Munich limekuja siku 3 kabla Bayern Munich haikurudi uwanjani jumatano hii kwa nusu-finali ya kombe la shirikisho la dimba la Ujerumani (DFB) dhidi ya hiyo hiyo wolfsburg iliowalaza juzi Bremen.

Baada ya Bayern Munich kushindwa nyumbani na Anderlecht ya Ubelgiji katika kombe la UEFA ingawa imefaulu kingiaduru ijayo na pigo hili la pili huko Cottbus, Bayern munich ina wiki ya misukosuko.

Bremen nayo ilizabwa mabao 6-3 wiki iliotangulia na mabingwa stuttgart na ikatolewa kabisa katika champions League-kombe la klabu bingwa barani Ulaya na sasa kwa kushindwa jumamosi na Wolfsburg imeangukia nafasi ya 4 ya ngazi ya ligi huku Hamburg na Leverkusen zikichukua nafasi ya pili na ya 3 nyuma ya Bayern munich.

Kocha wa Bremen Thomas Schaaf amesema :

"Hatuna haja ya kudai mambo ni mazuri.Isitoshe,hatuhitaji kuambiwa ah, mlicheza hatahivyo uzuri.Nadhani ,kila mmoja anahitaji kufurahia ushindi lakini sisi hatukupata ushindi huo wiki hii."-alinun'gunika kocha wa Werder Bremen-Thomas Schaaf.

Kocha wa Wolfsburg na zamani Bayern munich Felix Magath aliueleza ushindi wa timu yake dhidi ya Bremen kuwa uliostahiki.Alisema:

" Nadhani tuikisema kwa ujumla, sio hatukustahiki ushindi,kwani kipindi cha pili baada ya kuongoza kwa bao 1 ,tulipata nafasi za kurudisha ghafula mashambulio na kuweza kutia bao jengine."

Ama katika La Liga-Ligi ya Spain, FC Barcelona iko pointi 7 nyuma ya viongozi wa Ligi-Real Madrid.Lakini licha ya kuongoza mara 2, Barcelona ambayo itacheza na Schalke ya Ujerumani katika duru ijayo ya champions League-kombe la klabu bingwa barani ulaya, ilimudu sulubhu 2:2.Bao la kwanza la barcelona dhidi ya Almeria lilitiwa na Bojan Krkic mnamo dakika ya 17 ya mchezo kabla simba wa nyika Samuel eto'o kutia bao lao la pili.Jumamosi,Real Madrid ilipoteza pointi 3 kwa kulazwa bao 1:0 na Deportivo La Coruna.

Katika Serie A au ligi ya itali,Inter milan iliopigwea kumbo kabisda nje ya champüions league, inaendelea kutamba nyumbani.mwishoni mwa wiki Inter iliikomea Palermo manao 2:1 wakati mahasimu wao wakubwa katika kinyan'ganyiro cha taji la ubingwa AS roma walitamba mbele ya AC milan kwa ushindi wa mabao 2:1.Juventus Turin inafuata nafasi ya 3 katika ngazi ya Ligi kufuatia ushindi wao nyumbani wa bao 1:0 dhidi ya Neapel. Cagliari inaburura mkia wa ligi.