Lipumba: ′Seif alifanya kosa kujitangazia matokeo′ | Matukio ya Afrika | DW | 04.05.2017
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Mzozo CUF

Lipumba: 'Seif alifanya kosa kujitangazia matokeo'

Mgogoro unaoendelea ndani ya Chama cha Wananchi CUF umepiga hatua nyingine  baada ya viongozi wawili wakuu, mwenyekiti Ibrahim Lipumba na Katibu Mkuu, Seif Sharif, kutoa hadharani kauli zinazokinzana.

Sikiliza sauti 03:21
Sasa moja kwa moja
dakika (0)

Mahojiano na mchambuzi Hussein Sengu

Lipumba akizungumza na chombo kimoja cha habari ametofautiana na Maalim Seif akisema ni afadhali Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC), Jecha Salim Jecha, aliyefuta matokeo ya uchaguzi wa Zanzibar kuliko Maalim Seif aliyejitangazia matokeo. Anasema Seif alifanya kosa kubwa kujitangazia matokeo. DW imezungumza na mchambuzi wa masuala ya siasa kutoka Tanzania Bwana Hussein Sengu kuhusu hali hiyo ya vuta nikuvute katika chama.

Sauti na Vidio Kuhusu Mada

Matangazo

IJUE DW

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com