1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Lebanon yaanza kuwarejesha wakimbizi wa Syria

Lilian Mtono
26 Oktoba 2022

Mamia ya wakimbizi wa Syria wanaoishi Lebanon wameanza kurejeshwa nchini mwao hii leo, likiwa ni kundi la kwanza la wakimbizi wanarejea Syria chini ya mchakato ulioandaliwa na Beirut.

https://p.dw.com/p/4Igmf
Syrische Flüchtlinge im Libanon
Picha: Bilal Jawich/Photoshot/picture alliance

Mpango huo unafanyika huku kukiwa na wasiwasi kutoka kwa makundi ya haki za binaadamu ambayo yanasema huenda una vipengele vinavyowalazimisha wakimbizi hao kurudi nchini mwao.

Soa Zaidi:Amnesty: Wanaorudi Syria wanateswa na kubakwa

Karibu wakimbizi 700 wa Syria waliokubali kurudishwa walionekana asubuhi ya leo wakiwa wamebeba masanduku, majokofu, majenereta na hata mifugo kama kuku tayari kwenda kuanza upya maisha baada ya vita.

Mamlaka za Lebanon zinasema mpango huo wa kuwarudisha wakimbizi waliokubalia kuondoka kwa hiyari unaratibiwa na shirika la kitaifa la Usalama.

Syrische Flüchtlinge im Libanon
Baadhi ya wakimbizi wa Syria wakiwa wamepakia baadhi ya vifaa vyao tayari kwa kuanza safar ya kurejea nchini mwao.Picha: Bilal Hussein/AP/picture alliance

Ingawa vita vya wenyewe kwa wenyewe vilivyodumu kwa miaka 11 nchini Syria kwa kiasi kikubwa vimetulia, lakini Umoja wa Mataifa unasema machafuko ambayo hujitokeza na hatari ya watu hao kukamatwa na kufungwa vizuizini bado vinafanya mazingira kutokuwa salama kwa wakimbizi hao.

Shirika la kimataifa la wakimbizi limerekodi zaidi ya wakimbizi 800,000 wa Syria wanaoishi nchini Lebanon. Wakimbizi hao walikimbia mapigano ya wenyewe kwa wenyewe nchini mwao, vilivyozuka baada ya maandamano ya kumpinga raisi Bashar al-Assad mnamo mwaka 2011. Kiwango cha juu kabisa cha wakimbizi nchini Lebanon huenda kikafikia milioni 1.2.

Mwaka 2018 kulifanyia mpango kama huo wa kuwarejesha wakimbizi wa Syria, ambao ulishuhudia watu 400,000 wakirejeshwa, lakini ulisimamishwa baada ya mlipuko wa janga la UVIKO-19. Rais anayeondoka madarakani Michel Aoun aliuanzisha tena mwezi huu na kuanza utekelezwaji Jumatano hii.

Wasyria wengi bado wanaishi kwenye mahame baada ya makazi yao na miundombinu ya umeme na maji kuharibiwa vibaya.

Mashirika: RTRE