LAHORE:Blair ameiahidi Pakistan msaada zaidi kupiga vita ugaidi
19 Novemba 2006Matangazo
Uingereza na Pakistan zimeahidi kuendelea kushirikiana kwa miaka mingi ijayo ili kupiga vita ugaidi na itikadi kali za kidini. Waziri mkuu wa Uingereza Tony Blair na rais Pervez Musharraf wa Pakistan walitoa taarifa hiyo,baada ya kukutana katika mji wa Lahore nchini Pakistan. Majadiliano ya viongozi hao hasa yalihusika na masuala ya kuchangia habari za upelelezi, kupambana na Wataliban waliochomoza upya nchini Afghanistan na kupanga miradi mipya yenye mtazamo wa wastani katika elimu ya kiislamu nchini Pakistan.