1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaBenin

Kura zaanza kuhesabiwa Benin baada ya uchaguzi wa rais

13 Aprili 2026

Kura zinahesabiwa nchini Benin baada ya kufanyika uchaguzi wa rais jana Jumapili ambao Waziri wa Fedha wa nchi hiyo Romuald Wadagni inaaminika atashinda.

https://p.dw.com/p/5C4Q8
Benin, Cotonou 2026 | uchaguzi wa rais
Tume ya Uchaguzi ya Benin imesema kwa jumla uchaguzi wa Jumapili 12.04,2026 ulifanyika kwa amani. Picha: Olympia De Maismont/AFP

Ikiwa atatangazwa mshindi atamrithi Rais Patrice Talon ambaye amemaliza muda wake madarakani wa mihula miwili ya miaka mitano.

Wadagni ambaye ameungwa mkono pia na Rais Talon, anamwagiwa sifa kwa usimamizi mzuri wa uchumi katika kipindi cha muongo mmoja uliopita licha ya taifa hilo kukabiliwa na uhalifu wa makundi ya itikadi kali.

Mwanasiasa huyo anayeungwa mkono na vyama viwili tawala anakabiliwa na upinzani wa wastani kutoka kwa Paul Hounkpe, ambaye kampeni yake haikuwa na msisimko na alinusurika kukosa idadi inayohitajika ya udhamini ili kushiriki uchaguzi.

Mkuu wa Tume ya Uchaguzi ya Benin, Sacca Lafia, amesema uchaguzi ulifanyika kwa amani licha ya madai kadhaa madogo yaliyoripotiwa na asasi za kiraia. Matokeo ya awali ya uchaguzi huo yanatarajiwa baadaye wiki hii.