1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kundi la wanamgambo la ADF lawauwa watu watatu Uganda

Amina Mjahid
27 Desemba 2023

Msemaji wa jeshi la Uganda, UPDF, Felix Kulayigye, amesema watu watatu wameuwawa katika shambulizi linalodaiwa kufanywa na wanamgambo wa kundi la Allied Democratic Forces ADF Magharibi mwa taifa hilo.

https://p.dw.com/p/4acB7
Uganda | Amiri jeshi Mkuu na Rais wa Uganda Yoweri Museveni
Amiri jeshi Mkuu na Rais wa Uganda Yoweri MuseveniPicha: ABUBAKER LUBOWA/REUTERS

Wanamgambo hao wanasemekana kuushambulia mji wa Kamwenge Jumatatu jioni na kumuua bibi wa miaka 75 na wajukuu wake wawili kabla ya kuchoma miili yao. 

Soma pia:Jeshi la Uganda latangaza donge nono kuwanasa ADF

Kulayigye amesema jeshi la UPDF inaendelea kuwasaka wote waliohusika na mauaji hayo.

Eneo kulikofanyika mauaji hayo limezungukwa na mbuga mbili kubwa za wanyama na kuna hofu kwamba kisa hicho huenda kikawatia hofu watalii na kuathiri sekta ya utalii inayochangia kiwango kikubwa cha uchumi wa taifa hilo.